Tuesday, 27 January 2009

Watumia dawa za kulevya hawatakiwi CHAN


Shirikisho la soka barani Africa (CAF) limesema litakuwa makini mno katika swala la kupiga vita utuamaji wa dawa haramu katika mkichezo kwenye michuano ya mataifa bingwa barani Africa (Chan) itakayofanyika huko nchini Ivory Coast mwezi ujao
Katibu mkuu wa shirikisho la soka hapa nchini (TFF) Fredrick Mwakalebela amesema CAF watakuwa wakipima wachezaji wawili kwa timu yeyote ile wakati wa michuano hiyo na kuwapima kama wanatumia dawa hizo haramu hata kama mchezaji akiwa kwenye bechi si anaecheza tu na katika hatu ya nusu fainali idadi ya kupimwa kwa wachezaji itaongezeaka hadi kufikia watatu badala ya wawili
CAF inataka nchi zote zitakazoshiriki michuano hiyo ya CHAN zinatakiwa kuwaeleza kwa kina wachezaji wao kuhusu dawa hizo haramu za kuongeza nguvu michezoni
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu huyo wa TFF, amesema tayari wamepatiwa mkataba wa kukubali kufanywa kwa uchunguzi kwa wachezaji watakaokuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ta Tanzania (Taifa Stars)
Moja ya adhabu ambayo itatolewa ni pamoja na kusababisha kuondolewa kwenye mashindano hayo yaliyopangwa kuanza februari 22 mwaka huu, na wachezaji wote hata walio majeruhi watafanyiwa uchunguzi huo.
Uchunguzi huo utafanywa katika vipindi tofauti vya mashindano hao ambapo awamu ya kwanza itafanyika wakati wa michezo ya awali ya mashindano hayo na awamu nyingine itafanyika wakati wa hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

No comments: