Wednesday 21 May 2008

Ni vita nyingine Chelsea Vs Man Utd

Ama kwa hakika waweza kusema eti ni vita lakini si jui kama kweli ni vita ni mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo timu za England tu ndugu hawa watakapoumana huko mjini Moscow ni RUSSIA
Chelsea inacheza na Manchester United katika mchezo huo wa kihistoria ambao dunia nzima wanautazama kwa hisi tofauti
Manchester United wao ni mabingwa wa England na Chelsea ni washindi wa pili na ukiangalia kwa kipindi cha hivi karibuni Chelsea imekuwa ikiifunga sana Manchester United sasa hatuajui leo mambo yatakuwaje ? All da Best all

Saturday 10 May 2008

Taifa Cup yawakumbusha watu nyumbani

Michuano ya soka kwa timu za mikoa inayoendelea hapa jijini Dar es salaam inawakumbusha watu nyumbani kwamaana kila mtu anaenda uwanjani kuangalia michezo hiyo basi huishangilia timu ya mkoa wake wa asili
kitu hicho kinawafanya watu wengine wakumbuke mbali sana huku hata baadhi ya watu ambao kwa kawaida huwa hawaonekani uwanjani basi hivi sasa utawakuta tena wengine wakidiliki hata kuongea lugha ya kabila lao
Hivi karibuni wakati timu ya Mkoa wa Tanga (Tanga Stars ) ilipocheza na timu ya mkoa wa Kagera (Rwelu Eagles) alionekana mwanamuziki maarufu sana hapa nchini wa bendi ya The Kilimanjaro (wananjenje) Waziri Ally alipokuwa ameketi kwenye jukwa la watu mashuhuri na bila aibu yeyote ile alikuwa akiishangilia timu ya mkoa wake wa asili Tanga
tena imefikia kipindi hadi watu sasa wanataniana sana tena kupita kisi huku baadhi ya watu wakinukuliwa kusema `` ebwana Taifa Cup inauma sana tena kupita Simba na Yanga'' hizo ni timu kubwa hapa Tanzania ambazo zinamashabiki kila kona ya Tanzania lakini sasa hivi wala kila mtua naangalia timu ya mkoa wake
Siku ya tano pale timu ya mkoa wa Ruvuma walipocheza na Kigoma Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia Radio yake ya TBC Taifa ilitangaza mchezo huo moja kwa moja toka uwanja wa Taifa hapa Dar es es salaama na watangaji wake walikuwa wawili na wote ni waasili ya mikoa hiyo miwili basi ilikuwa kazi kila mtu akitangaza alikuwa akivutia kwake basi raha tupu
Watangazaji hao walikuwa Buruani Muhuza (Kigoma) na Cliford Ndimbo (Ruvuma) sasa kazi ilikuwa si ya mchezo kila mtu akikamata kipaza sauti (microphone) basi lazima japo kidogo ataje baadhi ya mitaa ya mkoani kwao == kwa mfano yeye Baruani alionekana akiitaja waziwazi mitaa ya ujiji, Kazura Mimba hadi Majengo mpaka kibondo hiyo ni mmoja ya wilaya ya mkoa huo wa Kigoma
Sasa kazi ikawa kwa Ndimbo nae akaanza kuitaja mitaa ya kwao kama Bomba mbili ,Kipera, Mfaranyaki basi we acha tu raha tupu pale mtu anapokumbuka kwao anatamani awe pale lakini haya yote ni katika TAIFA CUP
Na sio wao tu bali kila mitaa kila mtu anajivunia timu yao == kiongozi mmoja wa timu kubwa hapa nchini alilazimika kusimama kwenye jukwa kuu la Uwanja wa Taifa na kwaambia mashabiki wa soka waliojana kwenye jukwa hilo wakifuatilia mchezo kuwa yeye kamwe hatoshabikia timu tatu za hapa Dar es salaam (Yaani timu za ILALA ,KINONDONI na TEMEKE ) kwamaana ana kwao na kusema nyumbani ni nyumbani hata kama ni chini ya mti lakini ni nyumbani lazima ajivunie na kwamwe hatoshangilia timu za hapa au za mkoa mwingine kwamaana kufanya hivyo ni sawa na kuwakana ndugu zake pamoja na familia yake na yeye aitwe msaliti
Nadhani hakuna anaetaka kuwa msaliti hata mimi ndugu yenu ama rafiki yenu nilienda uwanjani pale timu ya kwetu ya Mkoa wa TANGA ilipocheza na Kagera lakini bahati haikuwa kwetu wakatufunga kwa bao moja bila na wakatutoa katika mashindano hayo ya kombe la Taifa lakini hakuna tabu ipo siku nasi tutafanya vyema tu sawa tutaonana kwenye michuano ya vijana ya copa coca cola lazima tulipe kisasi lakini roho inauma sana unapoona timu yako ya mkoa ikitolewa ===== Hongera kwa timu zote zilizofanikiwa kutinga hatua ya pili == Tanga tunajipanga upya tukija sasa ni tishio na hongera sana timu ya wajomba zangu wa RUVUMA -- KAZENI BUTI kwamaana damu ni nzito tena kuliko maji na mama na baba ni Mungu wa dunia bila mama hakuna kitua najua mama yangu alifurahi sana siku ile timu ya mkoa wake wa asili ulipoilambisha mchanga timu ya mkoa wa Kigoma na nyimbo za kingoni na kinyasa bila kusahahu kimatengo ziliimbwa sana kama `` Tumpambe leleno tumpambe , tumpambe leleno tumpambe maua '' we ! we acha tu ndugu yangu

Tuesday 29 April 2008

Simba hoi kuichunglia michuano ta Kimataifa == Prisons hiyo == kukwa pipa

Timu ya Simba imekosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani baada ya kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa 2007 - 2008
Inakuwa adimu mno kwa soka la Tanzania kuzishuhidia timu za Simba na Yanga kukosa nafasi hiyo lakini hiyo imewezekana msimu huu kwamaana timu ya Prisons ilionyesha inataka nafasi hiyo toka kuanza kwa michuano hiyo Septemba 2007
Katika michezo ya mwisho la ligi hiyo Yanga ilitoka sare ya bila kufungana na watani wao wa jadi timu ya Simba huku Tanzania Prisons ikiifunga Polisi Morogoro kwa bao 1-0 lilotiwa kimiani na Mshambuliaji Shaaban Mtupa
`` Ninafuraha sana kuona timu yangau ya Prisona ikifanikiwa kushiriki michuano ya kimataifa (Kmbe la Shirikisho barani Africa) lakini hiyo haikiwa nia yetu tulitaka kuwa mabigwa wa mwaka huu hapa nchini'' amenena Mtupa
HONGERA SANA YANGA PAMOJA NA PRISONS

Monday 31 March 2008

Baadhi ya Wana TBC wakiwa katika sherehe ya Uzinduzi ya TBC

Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) wakiwa wamevaa sare katika shereshe ya uzinduzi wa shirika hilo hapo March 26/ 2008, katika viwanja vya TBC 1 jijini Dar Es Salaam , kutoka kushoto Lusajo Mwakabuku(Mtangazaji- TBC International) Chriss Mfinanga(Camera Man TBC 1) Cliford Ndimbo , Baruani Muhuza na Evance Mhando ( Mr Names ) wote ni watangazaji na waandishi wa habari TBC

Saturday 29 March 2008

MAMBO YA UZINDUZI WA TBC

Hayo ni mambo ya Uzinduzi wa Shirika la Utangzaji Tanzania (TBC) mambo hayo yalifanyika kwenye viwanja vya TBC1 zamani TVT,unaowaona hapo kutoka kushoto ni Judica Losai, Lusajo Mwakabuku,Evance Mhando , Cliford Ndimbo na Baruani Muhuza wote niwafanyakazi wa TBC