Tuesday 22 December 2009

Kesho ni vita ya Wakenya kwenye Shamba la bibi

Makocha wa timu za SOFAPAKA NA TUSKER zote kutoka Kenya wametambiana kushinda katika mchezo wao wa NUSU FAINALI wa michuano ya kombe la TUSKER Mchezo utakaofanyika hapo kesho katika uwanja wa UHURU Jijini DSM.
Katika mchezo huo wa nusu fainali timu itakayoshinda itakutana katika fainali mshindi wa mchezo kati ya SIMBA au YANGA zinazotarajia kucheza alhamisi wiki hii.
Kwa upande wake kocha wa timu ya TUSKER James Nandwa amesema makosa yaliofanyika katika mchezo na YANGA hayatajirudia tena kwani wachezaji wake wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo na wamejinda kushinda.Kocha wa mabingwa wa Kenya msimu huu timu ya Sofapaka Robert Matano amesema msimu huu Tusker ni wao na hapo kesho wanaenda kushinda tu mchezo huo sio kingine.

Nyota Simba hati hati kuikosa Yanga

Bado kichwa kinawauma wakuu wa bechi la ufundi la Simba kutokana na wachezaji wake mahiri wanne kuwa majeruhi na kutia hofu kama wanaweza kucheza mchezo wa nusu fainali wa kombe la TUSKER dhidi ya watani wao wa jadi wa soka la Tanzania Yanga.
Mchezo huo utachezwa siku ya Alhamis siku moja kabla ya sikuku ya X-masss kwenye dimba la Taifa (Shamba la Babu) na wachezaji ambao ni majeruhi hadi leo ni pamoja na nahodha Nico Nyagawa,Haruna Moshi Boban,Emmanuel Okwi na kiungo Uhuru Selemani ambae tayari imeshathitika kuwa hatocheza mchezo huo.
Meneja wa timu hiyo ya Simba Innocent Njovu amesema bado hawajui chochote kama wachezaji hao watacheza mchezo huo siku ya Alhamis au la ila bado wanaendelea na matibabu.
Njovu amesema mustakabali wa swala hilo litajulikanika hapo kesho kama wachezaji hao watacheza mchezo dhidi ya Yanga au hawatocheza.

Monday 21 December 2009

Yanga na Simba kukipiga Taifa Mpya nusu fainali ya Tusker

Shirikisho la soka hapa nchini (TFF) kwa kushirikiana na waandaaji wa michuano ya kombe la Tusker wamesema mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano hiyo baina ya watani wa jadi wa soka la Tanzania Yanga na Simba utapigwa kwenye dimba la Taifa (Shamba la babu).
Pamoja na kusema hivyo TFF imeweka wazi viingilio vya mchezo huo ambayo hazina tofauti na michezo mingine ya timu hizo mbili zinapokutana kwenye michuano mbali mbali.
Kiingilio cha juu siku hiyo ni elfu 40 huku kiingilioa cha chini kikiwa ni elfu 5.
Mchezo huo wawatani wa jadi utapigwa siku ya Alhamis Desemba 24 siku moja kabla ya sikuku ya xmass, mchezo huo utatanguliwa na mchezo baina ya wakenya watupu timu za Sofabaka na Tusker.
Msemaji wa TFF- Florian Kaijage amesema kuwa wao walishindwa kusema mapema kuwa mchezo huo utachezwa kwenye dimba la Taifa kwasababu uwanja huo unamilikiwa na Serikali lakini sasa kila kitu kipo safi.

PST na TPBO watofautiana kuhusu mpinzani sahihi wa Cheka


Chama cha ngumi za kulipwa nchini (TPBO) kimekanusha taarifa za kuwepo kwa dhuluma katika pambano la ngumi za kulipwa ambapo bondia FRANCIS CHEKA alibadilishiwa mpinzani siku moja kabla ya pambano.
Utata mkubwa juu ya pambano hilo uliibuka mara baada ya kuwepo kwa taarifa za kutowasili kwa bondia huyo hali iliyowashitua wapenzi wengi wa masumbwi ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa pambano hilo.
Hata hivyo pambano hilo lilifanyika ambapo FRANCIS CHEKA alipewa mpinzani toka Brazil na kumchakaza mpinzani wake huyo anaeitwa ISAACK TARAVES kwa KNOCK OUT katika raundi ya pili na kufanikiwa kutetea taji lake la IBO na WBC.
Rais wa TPBO YASSIN ABDALAH amesema kuwa uamuzi wa kubadilisha bondia ulitokana na kuchelewa kwa hati ya kusafiria ya bondia HENRIQ ARECO ambaye awali alitakiwa kupigana na Cheka.
Kauli hiyo inatofautiana na ya Rais wa shirikisho lingene la masumbwi ya kulipwa hapa nchini PST – Emmanuel Mlundwa ambae aliwambia mashabiki siku ya pambano kuwa bondia huyo hakua kwasababu ni mzee, sasa tuamini la nani … ni mzee au alikosa hati ya kusafiria…..

Wadau wa masumbwi wanadai kuwa huo ni ufisadi sasa mimi siju …

Friday 18 December 2009

Hayo ndio mafunzo ya FIFA

Wapiga picha wakiwa na mwalimu wao Erick toka Ufaransa baada ya kumalizika mpira.
Sawa kaka leteni picha zenye kiwango ... hayo ndio mambo ya FIFA ... huyo ni mpira picha wa TBC1 Samwel Mshana akiwa na mwenzie Nicholaus Mbaga.

aaahhh kaka Jacob Mani lete vitu..... unatisha
Wapiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakipiga picha wakati wa mafuzo ya vitendo ya kupiga picha za mpira wakati timu ya Simba ikicheza na timu ya SOFA PAKA ya Kenya kwenye michuano ya kombe la Tusker.
Wapiga picha hao pamoja na watangazaji wa mpira wa Radio na TV na wasimamizi wa Matangazo toka TBC na Chanel Ten wanapata mafuzo ya wiki moja yaliyoandaliwa na shirikisho la la soka Dunia (FIFA) jinsi ya kupiga picha na kutanga mpira pamoja na jinsi ya kusimamia na kuendesha matangazo ya moja kwa moja yaan LIVE ya mpira wa miguu.


Saturday 22 August 2009

Sendeu aula YANGA


Kulia aliezibwa na Camera ndie Louis Sendeu akiwa anava microphone akijianda kumuhoji mchezaji wa mpira wa Kikapu wa Kitanzania anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA Hasheem Thabeet kwenye kipindi cha kila wiki cha Michezo cha kwenye Luninga kinachoitwa MEZA YA MICHEZO kinachorushwa na Television ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayoitwa TBC1 hapo August 16/ 2009.
Hii leo jumamosi 22 August 2009 baada ya kupita wiki moja Louis Sendeu ametangazwa na timu ya ligi kuu Tanzania bara ya YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB (YANGA) kuwa msemaji wa timu hiyo ikiwa siku moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu mpya wa 2009 - 2010.
Yanga ni miongoni mwa timu zilizochelewa kutimiza azimo la Bagamoyo la kila timu za ligi kuu Tanzania bara kuanzi msimu huu wa 2009 - 2010 kuwa na watendaji watu wa kuajiliwa.
Mwingine alieula Yanga ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Yanga Lawrence Mwalusako ambae yeye amekuwa katibu mkuu na mtunza pesa ni Godfrey Mwenje.
Sendeu anakuwa mwandishi na Mtangazaji wa pili toka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa msemaji wa timu ya ligi kuu wa kwanza alikuwa ni Cliford Ndimbo aliechukua cheo kama hicho kwenye timu ya Simba.
Kila la heli mwanahabari mwenzetu Louis Sendeu katika ajira nyingine pamoja na Cliford Ndimbo.

Tuesday 18 August 2009

Hasheem ndani ya TBC









Mchezaji mpira wa kikapu wa Kitanzania Hasheem Thabeet anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA katika timu ya MEMPHIS GRIZZLES ya Tenesse akihojiwa na mwandishi na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Evance Mhando.
Mahojiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za TBC1 Mikocheni Jijini Dar es salaam siku ya jumapili August 16/ 2009 saa nane mchana ambapo Hasheem alienda kutembelea ofisi hizo na kushiriki kwenye kipindi cha wiki cha Michezo kinachoitwa Michezo Yetu kilichoendeshwa na Evance Mhando (Mr Names).
Pamoja na yote Hasheem aliwataka vijana wa Kitanzania kujitahidi kwenye michezo pia na kutilia mkazo swala la Elimu na kutokata tamaa mapema kwenye kila jambo wanalolitaka katika Maisha yao.


Tuesday 11 August 2009

St George yamtosa rasmi Ivo Mapunda


Timu ya ST George ya Ethiopia imesitisha mkataba wake na kipa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Ivo Mapunda aliekuwa akicheza soka la kulipwa kwenye timu hiyo ya Addis Ababa.
Ivo alijiunga na timu hiyo ya ligi kuu nchini humo akitokea timu ya Yanga Africa ya hapa Tanzania mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2008 na kuingia nayo mkataba wa miaka miwili.
Akiongea kwenye kipindi cha michezo cha kila siku cha Radio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inyoitwa TBC Taifa Ivo amesema yeye alirudi nyumbani kwaajili ya mapumziko ila ameshituka kupata habari hizo.
Habari hizo amezipata kwa njia ya Email jioni ya leo jumanne August 11/ 2009 ambayo imetumwa na kocho wa timu hiyo ya ST George Msebia Micho ambae kwa mujibu wa Ivo haina maneno mengi zaidi ya kusema wamestisha mkataba wake.
Akiongea kwenye kipindi hicho cha michezo cha TBC Taifa Ivo amesema kwa sasa atakachofanya yeye ni kufuatilia maslahi yake maana alipojiunga na timu hiyo aliingia nayo mkataba wa miaka miwili na kipindi hicho bado hakijaisha.
Akizungumzia kuhusu kwa sasa ataenda wapi kucheza soka maana hapa Tanzania dirisha la usajili limeshafungwa amesema mameneja wengi wa timu mbalimbali hapa barani Africa wamekuwa wakimsaka na sasa ataanza rasmi kufanya nao mazungumzo.

Friday 31 July 2009

Mkuu wa makapela apata jiko .... wengine vipi ....


Mwandishi wa michezo wa magazeti ya The Guardian ltd Jimmy Charles (kulia) akimvisha pete mkewe Ruth Lugoe ambaye alifunga nae ndoa katika kanisa katoliki la Boko Dar es salaam jana

Wednesday 18 February 2009

Maembe anatisha


Vitali Maembe ni mwanamuziki wa Kitanzania anaeimba kwa hisia sana na sasa naambiwa hayupo hapa nchini ameenda nchini Norway ambako anafanya kazi ya kufundisha Muziki na lugha ya Kiswahili
Aliwika sana katika wimbo wake wa Sumu ya Teja lakini pia ana nyimbo nyingi kama vile Uwanja wa Taifa ambao aliuimba maalum kwa uwanja mpya wa taifa uliokabidhiwa hivi karibuni kwaTanzania na serikali ya China na zingine ni pamoja na Kiombwe, Africa shilingi tano
Mungu akubariki huko uliko kwa kila ulifanyalo

Huyu ndie alietunga Mjomba

Wengi hawajua kama Irine Sanga ndie mtunzi wa wimba uliowika kupita kiasi wa MJOMBA ulioimbwa na Mrisho Mpoto .... watu wanaupenda sana wimbo huo kutokana na ujumba mzito uliopo ndani yake .... sasa mama tunasubiri kitu kingine kikali zaidi ya kile maana unatisha

Sunday 15 February 2009

Mourinho ataka kurudi Chelsea



Kocha wa zamani wa timu ya Chelsea na kocha wa sasa wa timu ya INTER MILLAN ya Itali Jose Mourinho anasema yu radhi kurudi kwenye timu yake hiyo ya zamani ya Chelsea ili kuifundisha tena kwa mara ya pili

Mourinho amesema kama ukimuuliza unaweza kurudi tena siku moja Kuifundisha Chelsea jibu lake litakuwa ndio kwamaana anaipenda sana timu hiyo

Huu ndio uwanja wa Taifa


Baada ya kumalizwa kujengwa uwanja huu uliitwa uwanja mpya wa taifa baade ukaitwa uwanja mkuu wa taifa na sasa umepewa jina rasmi na kuitwa Uwanja wa Taifa
na ule uwanja wa taifa wa zamani unaitwa uwanja wa Uhuru

Shamba la bibi la badilishwa jina


Huu ni ulikuwa ukiitwa uwanja wa Taifa na baadae utakitwa uwnja wa taifa wa zamani na sasa umebadilishwa jina na unaitwa uwanja wa UHURU
Kaulia ya kubadilishwa jina imetolewa na waziri wa Habri utamaduni na Michezo Mh George Mkuchika

Friday 13 February 2009

Hapa ni Posta mpya kwa Wazungu




Hii picha imepigwa kwa juu ikionyesha maeneo ya Posta mpya majira ya saa tano asubuhi huku kama kawaida daladala hazikosekani na wakati mwingine hasa majira ya jioni kupata basi kwenda nakoenda kazi inakuwa ngumu sana na kama una mtoto inakubidi uondoke mapema na majira ya usiku kupata basi huku tabu ndiomaana tunakuita Posta kwa wazungu

Wawili washinda kwenda kuiona Taifa Stars huko Ivory Coast

WATEJA wawili wa benki ya NMB ambao ni Kagenge Geofrey wa Mbarizi , Mbeya na wa pili anatoka Tunduru mkoani Ruvuma anaeitwa Mandingo Mussa Issa wote wawili wamefanikiwa kushinda bahati nasibu ya kwenda nchini IVORY COAST kushuhudia michuano ya mataifa bingwa barani Afrika itakayoanza mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa MAWASILIANO wa benki ya NMB, JOSEPHINE KULWA, amesema kuwa benki hiyo inaendelea na mchakato wake wa kutoa nafasi kwa wateja wa benki hiyo kwenda kushuhudia michuano hiyo.
KULWA amesema benki hiyo itaendelea kutoa zawadi mbalimbali katika bahati nasibu hiyo ambayo itafanyika tena wiki ijayo,Jumla ya washindi watano wanatarajia kufaidika na bahati nasibu hiyo ya benki ya NMB kwenda Ivory Coast kuishangilia Taifa Stars

Thursday 12 February 2009

Bongo Star Seach yaanza


SHINDANO la kusaka vipaji linalojulikana kama BONGO STAR SEARCH limepangwa kufanyika kwa mara ya tatu ambapo wasanii wataanza kutafutwa kuanzia tarehe 21 mwezi huu jijini ARUSHA.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini DSM mkurugenzi wa BENCHMARK na mdhamini mkuu wa shindano hilo kampuni ya simu ya VODACOM GEORGE RWEHIMBIZA wana imani kuwa shindano la mwaka huu litakuwa na msisimko mkubwa.
PAULSEN amesema kila mkoa utatoa washiriki 4 ambapo jumla ya washiriki 48 watachuana vikali kumpata super staa.Mshindi atakayepatikana atapatiwa zawadi pamoja na kurekodi albamu mpya katika studio

Mabingwa Ulaya wainyuka England

Mshambualaji wa timu ya Taifa ya Hispania David Villa akipiga shuti kufunga goli la kwanza kenye lango la timu ya taifa ya England
Kiungo wa timu ya taifa ya England David Beckham akisalimiana kocha wake wa timu ya taifa ya nchi hiyo Fabio Capello mara baada ya mchezo wao dhidi ya Hispania ambapo timu yao ili lala kwa bao 2- 0
Matokeo mengine katika michezo ya jana ya kirafiki
Tanzania 0 Vs Zimbabwe 0
Angola 0 Vs Mali 4
Cameroon 3 Vs Guinea 1
Misri 2 Vs Ghana 2
Ufaransa 0 Vs Argentina
Ujeruamani 0 Vs Nayway 1
Africa Kusini 0 Vs Chile 2


Wednesday 11 February 2009

Hiddink achukua mikoba ya Scolari



Timu ya Chelsea imethibitisha rasmi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Urusi Guus Hiddink atakuwa kocha wa muda wa timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu na wiki ijayo atatambulishwa rasmi kwa wachezaji wa timu hiyo kuwa ndio kocha wao mpya atakaewafundisha hadi mwishoni mwa msimu huu
Mapema leo asubuhi Kocha huyo wa timu ya Taifa ya Urusi aliimbia Radio ya taifa ya nyumbani kwao Uholanzi kuwa wiki ijayo anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Chelsea.
Hiddink mwenye umri wa miaka 62 amechukua jukumu hilo baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Luiz Felipe Scolari kutimuliwa kazi

Voda Com wa mwaga mamilioni Kilimanjaro Marathoni



Kampuni ya simu za mikononi ya VODACOM imetangaza udhamni wake katika mashindano ya mbio fupi ya KILIMANJARO MARATHONI kwa kiasi cha shilingi MILIONI 50
Meneja wa udhamini wa kampuni hiyo , EMILLIAN RWEJUNA amesema kampuni hiyo imedhamini mbio hizo ili kuleta burudani .
Naye katibu mkuu wa shirikisho la riadha Tanzania, SELEMAN NYAMBUI amesema mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisimko kutokana na maandalizi yanayoendelea hadi sasa.
Mrembo wa Tanzania, NASREEM KARIM naye anatarajia kushiriki kwenye mbio hizo ambazo zitafanyika MACHI MOSI.

Hiddink kuchukua mikoba ya Scolari


KOCHA wa timu ya TAIFA ya URUSI, GUUS HIDDINK ameviambia vyombo vya habari nchini UHOLANZI kuwa wiki ijayo anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya CHELSEA.
HIDDINK mwenye umri wa miaka 62 anatarajia kuchukua jukumu hilo baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo LUIZ FELIPE SCOLARI kutimuliwa kazi hapo juzi
HIDDINK, amesema anachukua jukumu la kufundisha CHELSEA hadi mwisho wa msimu huu baada ya chama cha soka cha URUSI kumruhusu kufundisha timu zote mbili kwa wakati mmoja
Kocha huyo ambaye ni raia wa UHOLANZI ni rafiki mkubwa wa mmiliki wa klabu ya CHELSEA, ROMAN ABRAMOVICH na hivi karibuni anatarajiwa kwenda UINGEREZA kukamilisha kazi ya kwenda kuifundisha CHELSEA.

Adebayor apeta Africa atwa tuzo


Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Arsenal ya England kutoka nchini Togo, Emannuel Adebayor amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa AFRIKA wa mwaka 2008
Mchezaji huyo amechaguliwa kwenye sherehe zilizofanyika jijini Lagos nchini Nigeria hapoa jana na kuwashinda kiungo wa Ghana na timu ya Chelsea Michael Essien na kiungo wa timu ya Taifa ya Misri na timu ya National Al Haly Mohamed Aboutrika
Katika sherehe hizo zimeshuhudia nchi ya Misri ikichukua tuzo tano ikiwemo ya timu bora ya taifa, klabu bora ambayo ni National Al Haly , mashabiki bora ambao ni wa timu hiyo ya National Al Haly ambayo ni bingwa wa Africa kwa ngazi ya vilabu na tuzo ya mwisho ni ya kocha bora ambayo imeenda kwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo ya Misry (The Pharaos) Hassan Shihata
Emannuel Adebayor anaecheza soka la kulipwa kwenye timu ya Arsenal ya England mwaka uliopita wa 2008 aliweza kufunga magoli 30 kwenye mashindano mbali mbali aliyocheza ikiwemo ya klabu yake na timu ya taifa ya Togo (The Hawks)

Ngasa anauzwa zaidi ya shilingi milioni 100

Mwenyekiti wa timu ya YANGA ya jijini Dar es salaam IMANI MADEGA akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuondoka kwa timu hiyo hapo kesho Alhamis February 12/ 2009 kwenda nchini COMORO kucheza mchezo wa marudiano na timu ya ETOILE D`OR MIRONTSY ya nchini humo wa ligi ya mabingwa barani Africa
Katika mkutano huo MADEGA alisema waliwasiliana na timu ya LOV HAM ya nchini NOYWAY inayotaka kumnunua kiungo mshammbuliaji wa timu hiyo ila hawajajibiwa hadi sasa na kusema katika email waliyoitumia timu hiyo waliiambia Mrisho Ngasa wanamuuza kwa dolla laki moja za Marekani ( $10,0000) sawa na zaidi ya milioni 100 za Kitanzania

Monday 9 February 2009

Scolari OUT Chelsea .... wamtosa bila aibu

















Habari zilizoingia punde zinasema Timu ya CHELSEA yaEngland imemfukuza kazi kocha wake LUIZ FELIPE SCOLARI.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo umeandika kuwa kutimuliwa ghafla kwa SCOLARI kunatokana na kiwango na matokeo ya klabu hiyo kutoridhisha.

Taarifa hiyo inasema ili kudumisha changamoto ya mataji wanayowania wamelazimika kufanya hivyo na tayari mchakato wa kusaka kocha mwingine umeanza na atatangazwa haraka iwezekanavyo na kwasasa timu hiyo iko chini ya kocha msaidizi RAY WILKINS kwa muda.




Pompey wamtimua kazi Tony Adams





Timu ya PORTSMOUTH (Pompey) imemtimua kazi kocha wake TONY ADAMS kutokana na timu hiyo kufanya vibaya katika ligi kuu England

Timu hiyo ikiwa na kocha Adams aliiwezesha timu hiyo kushinda michezo miwili tu kati ya michezo kumi na sita iliyocheza katika ligi hiyo na tangu kocha huyo ajiunge kuifundisha timu hiyo mwaka jana mwezi Octoba

Kutokana na kufukuzwa Tony Adams sasa mikoba ya kocha huyo inachukuliwa na kocha wa timu ya vijana wa timu hiyo, Paul Hart ambaye ataifundisha kwa muda huku.

Hata hivyo kocha Adams amesisitiza kwa kusema kuwa kufanya vibaya kwa timu yake kumechangiwa na uongozi wa timu hiyo.


Ujio mpya Dar City



Ni kweli ujio mpya ndani ya jiji la Dar es salaam baada ya Taa za barabarani zinatotumia umeme wa Sola kuingia katika jiji hili la shangwe
Kwamaana hiyo naweza kusema Watanzania tumeanza kunufaika na jua letu linalotuchoma kila kukicha hapa BONGO
Taa hizo zimewekwa katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi (Bagamoyo Road) katika maeneo ya BAMAGA na katika makutano ya barabara za Mandela na Nyerere , Maeneo ya TAZARA
Tunaomba taa hizi ziwekwe katika jiji zima la Dar es salaam maana mara nyingi umeme ukikatika basi kunakuwa na vurugu tu maana taa hizo huwa hazifanyi kazi kabisa sasa kama taa za sola zikiwa nyingi najua fika kutakuwa hakuna vurugu hata kidogo

Sunday 8 February 2009

Wazo Tete inatisha....bonge la Kipindi TBC1




Hapa mzee wa Wazo Tete Dotto Athuman wa TBC1 akitoa maelekezo wa wanafunzi wa shule la Sekondari ya Loyola ya jijini Dar es salaam mua mfupi kabla ya kuingia kwenye mjadalawa Wazo Tete


Mzee wa Wazo Tete Dotto Athuman mara baada ya kurekodi kipindi akitoka kwenye ukumbi akiwa na vifaa kibao amevibeba ........ kazi ngumu ukiipata ndugu yangu ama sivyo we acha tu .... hongera kwa bonge la kipindi



Tuesday 3 February 2009

Henry Joseph na Emeh wakisaka maisha bora nchini Norway












By TBC Sports Desk
Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) na timu ya Simba Henry Joseph na mshambuliaji Mnigeria Emeh Izuchukwu wanaendelea kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye timu ya Molde FK iliyopo kwenye mjii wa Las Palmas inayoshiriki ligi kuu nchini Norway
Wachezaji hao wataendelea na majaribio na timu hiyo ya Molde FK kwa siku mbili zaidi kabla ya kwenda kwenye timu nyingine ya Tromso kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini humo
Hahari zinasema timu ya Molde FK imeonekana kuvutiwa mno na wachezaji hao ila ni mapema mno kusema kama wanaweza kupewa mkataba wa kuichezea timu hiyo
Na kocha wa timu hiyo ya Molde FK aliefahamika kwa jina moja tu la Kjeil amesema Henry Joseph ni mzuri mno kiufundi na kuvutiwa sana na kiungo huyo anaechezea timu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars)