Tuesday 27 January 2009

Watumia dawa za kulevya hawatakiwi CHAN


Shirikisho la soka barani Africa (CAF) limesema litakuwa makini mno katika swala la kupiga vita utuamaji wa dawa haramu katika mkichezo kwenye michuano ya mataifa bingwa barani Africa (Chan) itakayofanyika huko nchini Ivory Coast mwezi ujao
Katibu mkuu wa shirikisho la soka hapa nchini (TFF) Fredrick Mwakalebela amesema CAF watakuwa wakipima wachezaji wawili kwa timu yeyote ile wakati wa michuano hiyo na kuwapima kama wanatumia dawa hizo haramu hata kama mchezaji akiwa kwenye bechi si anaecheza tu na katika hatu ya nusu fainali idadi ya kupimwa kwa wachezaji itaongezeaka hadi kufikia watatu badala ya wawili
CAF inataka nchi zote zitakazoshiriki michuano hiyo ya CHAN zinatakiwa kuwaeleza kwa kina wachezaji wao kuhusu dawa hizo haramu za kuongeza nguvu michezoni
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu huyo wa TFF, amesema tayari wamepatiwa mkataba wa kukubali kufanywa kwa uchunguzi kwa wachezaji watakaokuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ta Tanzania (Taifa Stars)
Moja ya adhabu ambayo itatolewa ni pamoja na kusababisha kuondolewa kwenye mashindano hayo yaliyopangwa kuanza februari 22 mwaka huu, na wachezaji wote hata walio majeruhi watafanyiwa uchunguzi huo.
Uchunguzi huo utafanywa katika vipindi tofauti vya mashindano hao ambapo awamu ya kwanza itafanyika wakati wa michezo ya awali ya mashindano hayo na awamu nyingine itafanyika wakati wa hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Serengeti yaipa mamilioni tena Akudo







Kampuni ya bia ya Serengeti imeongeza udhamini wake kwa bendi ya muziki wa dansi hapa nchini ya Akudo na sasa udhamini huo ni wa milioni 200 toka ule uliopita wa mwaka jana uliokuwa wa milioni 150
udhamini huo pia utatumika katika kijitangaza bend pamoja na kufanya shughuri za kijami zitakazofanywa na kampuni hiyo ya bia ya Serengeti kwa kipindi hiki cha mwaka 2009



Monday 26 January 2009

Vigogo wa SADC wakutana Africa kusini kuiokoa Zimbawe


Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC wanaendelea na kikao chao cha dharura mjini PRETORIA, AFRIKA KUSINI kwa lengo la kutafuta njia za kutatua mgogoro wa kisiasa nchini ZIMBABWE.
Mkutano wa viongozi hao unafanyika kufuatia kikao cha hivi karibuni kati ya rais ROBERT MUGABE na MORGAN TSVANGIRAI kushindwa kufikia mapatano juuya mzozo wa kisiasa nchini ZIMBABWE
Akifungua mkutano huo mjini PRETORIA Mwenyekiti wa SADC Rais wa Afrika Kusini KGALEMA MONTLANTHE amesema ana matumaini kuwa viongozi wanachama wanaokutana hii leo watatumia fursa hiyo kuupatia suluhisho la kudumu mzozo wa kisiasa nchini ZIMBABWE ambao umesababisha adha kubwa kwa wananchi wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na matatizo ya kiuchumi.
MONTHLANTHE amesema awali ZIMBABWE ilikua mzalishaji mkubwa wa chakula na hata kusafirisha nje ya nchi lakini kwa sasa nchi hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula hali inayosababisha adha kwa wananchi wa nchini hiyo kutokana na mzozo huo wa kisiasa
Mkutano huu wa viongozi wa SADC utakua mkutano wa NNE kufanywa na viongozi hao, wakizungumzia mzozo wa ZIMBABWE tangu uchaguzi mkuu wa mwezi Machi mwaka jana uliokabiliwa na utata. Kikao cha leo pia kinatarajiwa kutoa tamko la pamoja juu ya mzozo huo wa ZIMBABWE

Villa Squad yaanza kujikomboa kutoshuka daraja

By Cliford Ndimbo (TBC)
Goli pekee lililofungwa na mshambuliaji Abu Ramadhani limetosha kabisa kuipa ushindi timu ya Villa Squad ya jijini Dar es salaam dhidi ya timu ya Polisi Morogoro na kuipa matumaini mema katika mzunguko huu wa pili wa ligi hiyo
Goli hilo lilifungwa katika dakika ya kumi ya mchezo kupindi cha kwanza katika mchezo ulikabiliwa na mvua kitu ambacho kilikuwa kikwazo kwa wchezaji kuonyesha soka safi
Matokeo hayo yameaanza kuleta moyo kwenye timu hiyo toka manispaa ya Kinondoni kama inaweza kubakia ligi kuu msimu ujao kwamaana toka mzunguko wa pili uanze timu hiyo imeshinda michezo miwili na kufungwa mchezo mmoja tu
Kwanza kabisa waliilaza timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya bao 2- 0 na kufungwa na mnyama Simba na leo wameifunga timu ya Polisi Morogoro
Kwa matokeo hayo sasa Villa Squad imefikisha pointi 14 lakini bado ipo kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja pamoja na timu za Polisi Dodoma na Polisi Morogoro ambazo zote zinachukungulia kaburi
Tusubiri kuona kama timu hizo zitashuka daraja au kupona sie yetu macho na masikio …. kusikia
Kesho ligi hiyo inaendelea kwa kupigwa mchezo mmoja tu kwenye dimba hilo holo la taifa la zamani (Shamba la bibi) ambapo mabingwa watetezi na vinara wa ligi hiyo Yanga watakaocheza na timu ya Mtibwa Sugar toka Morogoro

Yanga yapinga kumzuia Ngasa


Mwenyekiti wa klabu ya YANGA IMAN MADEGA amekanusha uvumi ulioena kuwa wamekataa kumruhusu mchezaji MRISHO NGASA kwenda kucheza soka la kulipwa nchi NORWAY
Akizungumza Jijini DSM MADEGA amesema klabu haiwezi kumruhusu mchezaji yoyote kwenda kucheza soka nje bila mawakala au klabu inayomtaka kufuata utaratibu.
MADEGA amesema hakuna makubaliano yaliyofanywa na Timu ya LOV- HAM ya NORWAY ambayo inamtaka mchezaji huyo.
Amesema January 23 timu hiyo ilituma maombi ya kutaka NGASA akafanye majaribio kwa muda wa wiki moja na si kumsajili moja kwa moja kama vyombo vya habari vilivyoripoti hapo awali
Amesema baada ya uongozi wa timu hiyo kukutana na kukamilisha utaratibu na timu hiyo NGASA ataondoka nchini kwenda kufanya majaribio mwezi huu wa January au February mwaka huu kisha atarudi nchini baada ya wiki moja.
Kuhusu NGASA kutoroka kambini MADEGA amesema NGASA yupo kambini na klabu ya YANGA na sasa anasumbuliwa na tumbo ndiyo maana hajaonekana mazoezini na ameaanza kuumwa leo na kukanusha habari zilizoenea kuwa ametoroka kwwenye timu hiyo

Mwanza kuna ziwa Iringa kuna mtoo





Awali mdau wetu Shabaani Kondo toka Iringa alisema Iringa kama Mwanza na sasa anasema kama Mwanza kuna ziwa basi Iringa kuna mtoo unaoitwa Ruaha
Wanairinga wanausifu sana mtoo huu na ni heshima kwao
Kama unavyoona kwenye picha baadhi ya wakazi wa Iringa wakichota maji kwaajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani na kuna watu wanavua samaki kwenye mtoo huu ........ basi raha tupu
Swali kwako kaka Kondo Lipuli ipo wapi kwa sasa imeshakufa? hebu tueleze kwa kina kuhusu hili ........

Sunday 25 January 2009

Unakumbuka JK alipodata kwa ushindi wa Stars


Ilikuwa Septemba mwaka 2006 kwenye dimba la Taifa la zamani (Shamba la bibi) pale timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) iliposhinda mchezo wake wa kwanza wa kimashindano baada ya miaka kumi chini kocha wake Mbrazil Marcio Maximo na ulikuwa mchezo wake wa kwanza wa mashindano akiwa kocha mkuu wa Taifa Stars
Rais Jakaya Kikwete alikuwepo uwanji siku hiyo kama mmoja wamashabiki wa Stars na mgeni rasmi alikuwa aliekuwa waziri wa habari utamaduni na Michezo ambae kwa sasa ni waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais anaeshughurikia Muuungano Mh Mohamed Seif Hatibu
kikosi cha Stars kilikuwa hivi
1, Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Mack Maxime, Salum Sued, Henry Joseph, Renatus Njohole, Athumani Idd, Gaudence Mwaikimba ,Said Maulid na Abdi Kassim, mmoja ya wachezaji walioingia ni Nizar Khalfan aliefunga goli l ushindi siku hiyo

Kiberiki vitani kesho

Ni mtihani mwingine tena kwa kocha Ken Mwaisabula wa kuinusuru timu ya Villa Squad isishuke daraja msimu huu hapo kesho pale timu hiyo itakapocheza na timu ya Polisi Morogoro
kocha huyo aliaanza kazi hiyo vyema katika duru hili la pili la ligi kuu Tanzania bara baada ya kuilaza Tanzania Prisons ya Mbeya bao 2 -o
Lakini kumbe sikio la kufa halisiki dawa wakalizwa na Mnyama Simba
sasa tusubiri kuona hapo kesho mfa maji anapotapatapa kutaka kujiokoa na itakuwa raha kwa makamu wa pili wa Rais wa TFF Ramadhan Nassib aliepata cheo hicho kupitia timu hiyo inayopigania kutoshuka daraja msimu huu

Toka anaanza kazi katika timu hiyo katika mzunguko huu wa pili kocha Ken Mwaisabula alishasema nia yake ni kuibakiza timu hiyo ligi kuu Tanzania bara sasa wadau wa soka wanasubiri kuona ataweza au jahazi litazama mbele yake?
kila la heli Villa Squad na Mungu awabariki
Hapo jana tuliona pesa zikishindwa kufanya kazi baada ya mamilionea Azam FC kulala mbele ya askali wa jeshi la kujenga taifa JKT Ruvu bwao 2 - 1
huo nimuendelezo tu kwamaana katika mchezo wa kwanza JKT Ruvu waliiza Azam FC kwa idadi hiyo hiyo ya magoli
ooh ooh ooh ooh pole sana ndugu zangu wauza unga na maji hapa Tz

Messi aikana Real Madrid

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Barcelona ya Hispania Muagentina Lionel Messi amekanusha habari zilizoenezwa eti yeye anampango wa kuihama timu hiyo na kujiunga na wapinzani wao wakubwa Real Madrid na kusema yeye hajui uvumi huo umeanzia wapi na nani alivumisha habari hizo
Akizungumza baada ya mchezo wa ligi ya Hispania kumalizika dhidi ya Numancia ambapo timu yake ilishinda bao 4 -1 Messi amesema yeye hanampango wa kuondoka Barcelona na hajui kama ipo siku ataondoka kwenye timu hiyo na kama ataondoka basi si matwakwa yake ni timu yake iamue kumuuza
Kinda huyo toka Kusini mwa America anasema toka alipokuwa mdogo malengo yake yalikuwa kuchezea Barcelona na anapenda kuendelea kubakia hapo katika maisha yake yote ya kucheza soka Sio Real Madrid tu wanaohusishwa na uhamisho wa Messi ila hata Inter Milan ya Italia nayo inasemekana ina nia ya kutaka kumsajili kijana huyo na hata kocha wake wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona amewahi kusema muda umefika kwa kipenzi chake hicho kuhamia Italia na kuachana na soka la Hispania

Friday 23 January 2009

Usikose Weekend hii

Usikose Asubuhi hii ya Mwishoni mwa juma kupitia TBC Taifa na mimi Evance Mhando aka Mr Names
Jumamosi tunazungumzia Michezo tu bila kusahau burudani nzuri ya muziki tofauti tofauti
Siku ya jumapili pata habari kemkem za kitaifa na kimataifa pia tunazungumzia mambo ya utamaduni na mila na desturi za Kitanzania na burudani haikosekani hata kidogo ..... ungana nami ili ujue na kuburudika

Ni ASUBUHI HII ya MWISHONI MWA JUMA na Evance Mhando ..... USIKOSE

Waarabu waitamani Chelsea



Taikuni wa kiarabu alieongoza mpango wa kuinunua timu ya Manchester City Dr Sulaiman al-Fahim pamoja na washirika wake wa Kijerumani wanampango wa kupeleka ombi la kutaka kuinunua timu ya Chelsea inayomilikiwa na bilione wa Kirusi Roman Abramovich
Wiki iliyopita Abramovich alikanusha habari zilizoenea eti yeye anampango wa kuiza timu hiyo aliyoinunua mwaka 2003 toka kwa tajili wa kingereza Ken Betis na kuifanya iwike baada ya kuwekeza kiasi cha paundi milioni 600 na kununu wachezaji wenye majina makubwa duniani kama Didier Drogba wa Ivory Coast
AL –FAHAM amesema haitakuwa rahisi kwa mtu mmoja kuinunua klabu hiyo lakini endapo wawekezaji wengine watajiunga pamoja kwa kuchanga pesa jambo hilo linawezekana.
Taikunu huyo anaemili kampuni ya Abu Dhabi United Group anasema yeye binafsi anajua fika kuinunua Chelsea ni kazi ngumu na haitakuwa bei rahisi na itawagharimu pesa nyingi huku mshirika wake toka Ujerumani Holger Haims akisema kila kitu kinawezekana na hawezi kuamini eti Chelsea haiuzwi kama wakitoa pesa nzuri kila kitu kinawezekana na watainunua tu timu hiyo ya Magharibi wa jiji la London

Taikuni wa Kiarabu aitaka Liverpool

Mmoja wawamiliki wa timu ya Liverpool Tom Hicks leo amefanya mazungumzo na Taikuni wa Kiarabu toka Kuwait aneitwa Nasser Al-Kharafi wakiangalia uwezekano wa tajili huyo kuinunua timu hiyo ya Merseyside
Habari zinasema taikuni huyo anampango wa kutoka kiasi cha paundi bilioni tisa ili kuinunua Liverpool huku wamiliki wa timu hiyo Tom Hicks na George Gillet wakikadilia kuwa timu yao inathamani ya kiasi cha paundi milioni 550
Wamarekani hayo hivi sasa hawapo kwenye maelewano mazuri toka wainunue timu hiyo February 2007 kw akiasi cha paundi milioni 218 na sasa wapo tayari kuiuza timu hiyo
Habari za kina kuhusu kuuzwa kwa timu hiyo zinasema mkurugenzi wa Bishara wa Liverpool Ian Ayre na mkurugenzi wa fedha Philip Nash wataenda msharaki ya kati ili kuendelea na mazungumzio hayo na kama itashindikana basi tajili huyo wa Kiarabu atanunu asilimia 50 za hisa za timu hiyo huku Tom Hicks na George wakisaliwa na asilimia 25 tu ndani ya Liverpool


Nkunda atiwa mikononi


By Zaituni Mkwama (TBC International Desk)
Kiongozi wa majeshi yaliyoungana kati ya majeshi ya RWANDA na Jamhuri ya kidemokrasi ya KONGO kufanya operasheni ya kuwasaka waasi amesema Kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya KONGO –DRC LAURENT NKUNDA amekamatwa.

Amesema NKUNDA amekamatwa nchini RWANDA alipokimbilia wakati akijaribu kuwazuia wanajeshi wa RWANDA kufanya operesheni hiyo.

Mapema wiki hii askari wa RWANDA wameingia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya CONGO ikiwa ni sehemu ya mkataba uliofikiwa kati ya nchi hizo mbili wa kupambana na kikundi cha waasi wa kihutu wa RWANDA wanaofanya mashambulizi yao kutokea DRC.

Askari Elfu TATU MIA TANO wa RWANDA wameingia mashariki mwa DRC kuungana na wanajeshi wa DRC kuwanyanganya silaha waasi wa kihutu wa kundi la FDLR

Mwazoni mwa mwezi huu mnadhimu mkuu wa jeshi hilo la waasi Jenarali BOSCO NTAGANDA alitoa maelezo ya kupinduliwa kwa NKUNDA kwa madi kuwa NKUNDA si kiongozi anayefaa kwa kikundi hicho kutokana na kuwepo kwa utawala mbaya.

Hata hivyo NKUNDA alikanusha taarifa hizo na kueleza kuwa mnadhimu huyo ana makosa ya kukiasi kikundi hicho kwa kutoa taarifa za uongo na hausiki na madai ya kutaka kumpindua.

Mwezi August mwaka jana waasi hao walianzisha mashambulizi Mashariki mwa DRC ambapo zaidi ya watu laki mbili na nusu walikimbia makazi yao kwa kuhofia vita.


====

Drogba apania kurudi kikosi cha Kwanza Chelsea


Pamoja na kutengewa kiasi kikubwa cha pesa na timu ya Manchester City ili kumsajili mshambuliaji wa timu ya Chelsea Didier Drogba ametangaza kuendelea kupigania namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Luiz Felipe Scolari
Habari za kina zinasema Drogba yupo kwenye mpango wa kubadilishwa na Mbrazil Robinho iliaende Chelsea na Muivory Coast huyo aende Man City lakini pia kunataarifa zinazosema mshambuliaji huyo atarejea kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea kesho jumamosi kwenye mchezo wa raundi ya nne wa kombe la FA dhidi ya timu ya Ipswich Town

Maradona wa Ulaya kuihama Pompey


Kiungo wa Croatian anaechezea timu ya Portsmouth ya England Niko Kranjcar (Maradona wa Ulaya) amethibitisha rasmi kuwa timu yake hiyo imekubali kumuuza mwishoni mwa msimu huu yaani kwenye majira yajayo ya usajili ya kiangazi
Timu za Arsenal na Tottenham Hotspurs ndio zinazopigana sana vikumbo kumuwania kiungo huyo na yeye mwenyewe Kranjcar anasema kwa sasa anasubiria kwa hamu kubwa uhamisho huo lakini atabakia Fratton Park hadi mwishoni mwa msimu huu
Pamoja na yote Kranjcar amekanusha habari zilizoenea zinazosema eti yeye ameongea na kocha wake wa zamani Harry Redknapp ili amsajili jambo ambalo amelipinga vikali na kusema mchezaji mwenzie wa nchi moja Luka Modric yupo kwenye timu hiyo ya Spurs na anacheza kwenye nafasi kama anayocheza yeye na inakuwa ingumu kwake kujiunga na timu hiyo

Thursday 22 January 2009

Nahodha wa Taifa Stars kwenda kusaka maisha Ulaya

By Luis Sendeu TBC
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) , Henry Joseph Shindika anatarajiwa kuondoka jumamosi wiki kwenda nchini NORWAY kwaajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini humo.Katibu mkuu wa shirikisho la soka la Tanzania (TFF) Fedrick Mwakalibela amesema mipango yote ya kwenda kufanyiwa majaribio katika klabu moja nchini humo imeshakamilika.Mwakalibela amesema kuondoka kwa mchezaji huyo kunafungua milango kwa wachezaji Wengine wa Tanzania katika kusa nafasi ya kucheza soka la kulipwa katika nchi za ulaya.
Mwakalibela pia ameelezea juu ya mchezaji Athuman Machupa ambaye naye anaondoka Jumamosi kwenda nchini DENMARK kufanya majaruibio katika klabu moja ambayo jina lake bado halijapatikana.Machupa ambaye amewahi kuichezea klabu ya Simba na timu ya taifa mara kwa mara alikuwa akichezea klabu ya Fanja iliyopo falme za kiaarabui katika michuano ya kombe la mafuta.Baadhi ya wadau wa soka hapa jijini Dar es salaam wamesema wachezaji wengi tu wa wengi wa timu ya taifa wanaweza kupata timu ya kucheza soka huko ulaya iwapo timu ya taifa, Taifa Stars itafanya vyema katika michuano ya mataifa bingwa barani Africa (CHAN) itakayofanyika mwezi ujao nchini IVORY COAST

Wednesday 21 January 2009

Na mimi nilikuwepo siku TBC ilipozaliwa

Siku hii ni ya kukumbukwa sana ilikuwa March 26/ 2008 siku ya uzinduzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na mimi nilikuwepo tukawa wote kwa kila jambo basi ilikuwa raha .... we acha tu .... siku hii tutaikumbuka siku zote

Swali .. nitajie majina ya hawa waliogeukia mbele

Aliesimama kushoto ni Shaaaban Kissu mkuu wa idara ya Habari na matukio TBC Taifa, je waliosimama kulia watatu wa kwanza na mmoja aliekaa kwenye kiti cha kwanza kulia ni akina nani? Ila wote ni wafanyakazi wa TBC , tuma jibu lako katika email hii modu80uk@yahoo.com, wafanyakazi wa TBC hawaruhusiwi kujibu

Soko kuu la Iringa





Hili ni soko kuu la Iringa hapa kila kitu poa hata Dogi inapatikana we njoo tu utapewa

AIG yaitosa Man United


Kampuni ya AIG ya Marekani inayoidhanini timu ya Manchester United ya England imakata kuongeza mkataba wa kuendelea kuidhamini timu hiyo mara baada ya mkataba wa sasa kumalizika mwaka ujao wa 2010
Kampuni hiyo ilitoka kiasi cha paundi milioni 14 katika mkataba wa miaka minne ambao unamalizika 2010 na leo AIG imesema haina mpango tena wa kuendelea kuidhamini timu hiyo

Hapa ni nyumbani kwetu

Huu ni uwanja wa timu ya Chelsea upo magharibi mwa jiji la LONDON ni kama nyumbani vile sisi mwenyewe wenyeji hapa tunapaita darajani wakati ule bwana raha tu
Wakati wa kaka Jose Mourinho kufungwa hapa ilikuwa ni ndoto lakini siku hizi hali ni tofauti kabisa .... inauma sana lakini tufanye nini inabidi tukubali matokeo
MUNGU yupo na ipo siku na sisi tutatesa tena

Eti wanasema Iringa kama Mwanza








Yule kaka yetu alieondoka kwenda Iringa anaeitwa Shaaban Kondo ametuletea picha hizi na kutupa taarifa za wakazi wa mjii huo wanaosema eti mjii wao hauna tofauti na mjii wa Mwanza (Rock City)




Sasa sisi wanatupo wote tunajiuliza hivi Iringa nako kuna ziwa? lakini hayo acha tuwaachie wenyewe wanyalukolo, Ndauli be ! unogile




Lakini kaka Shebby mbona hujatupa habari za baridi? maana hapo jana tulimuona Kaka Obama akiapa huku kukiwa na baridi kali na nilikuwa karibu na jamaa flani hivi akaniambia ile ni kama baridi ya Iringa sijui ni kweli au la!!! hebu ulizia Mafinga , Makambako hadi Njombe mambo yakoje huko?




Vipi mzee dogi linaliwa au bado mchecheto? hakuna shida we kula tu kaka maana kilichoumbwa na muweza wewe huwezi kukigomea maana kina kila baraka zote toka kwake


Sera kuu ya Obama ni kufufua Uchumi na vita dhidi ya Ugaidi

Barack Obama ameanza kazi kama Rais mpya wa Marekani kwa kukutana na wakuu wake wa ushauri wa mambo ya Uchumi na wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo ikiwa ni siku yake ya kwanza kufanya kazi kama Rais katika Ikulu ya White house

Akiapa kuchukua jukumu hilo la kuwa Rais wa 44 wa Marekani Obama alisema matatizo ya Uchumi na vita vya Afghanistan na Iraq ni mambo yake muhimu ya kwanza kuanza kuyafanyika kazi

Wakati hayo yakiendelea mjini Washington DC sherehe za zilikuwa zikiendelea katika baadhi ya mitaa ya mjii huo

Tuesday 20 January 2009

Obama akiapa kuwa Rais




Hapa Barrack Obama anaapa kuwa Rais wa 44 wa Marekani na kuwa Rais wa kwanza mwenye asili ya Africa

Historia yawekwa Marekani





Mambo ya kuapa kuwa Rais wa Marekani, sasa imetimia BARACK OBAMA ndie Rais mpya wa Marekani

Raha sana .....



Ni raha tena kupita kiasi mwaafrica anapotawala Dunia

Muda mchache kabla ya Obama kuapa kuwa Rais wa Marekani


Hapa ni punde tu kabla ya kijana Obama kuwa Rais wa Marekani akiwa na Rais anaemaliza muda wake George Bush pamoja na wake zao

Jinsi Historia inavyoandikwa kwa Obama




Si jui ni niseme nini maana Historia inaraha yake, hapa ni Woshington DC , angalia kijana alivyoshika bendera za nchi hiyo hapo katika ni umati mwingine ulijitokeza kumuona OBAMA akiapa na juu ni sehemu ambayo sherehe hizo zitafanyika
MUNGU MKUBWA na leo Historia imeandikwa ,Dunia kuongozwa na Mwaafrica tena kutoka Africa Mashariki huyo si mwingine ni BARACK OBAMA


Umati wajitokeza kumuona Obama akiapa

Umati huu unaouona umejitokeza ilikuona Rais mpya wa 44 wa Marekani BARACK OBAMA akila kiapo cha kuiongoza nchini hiyo kubwa Duniani

Obama imetimia , imetimia kweli kweli


Ilikuwa mwaka, ikiwa miezi,ikawa mwezi, ikawa wiki , ikawa siku na sasa bado saa chache tu kijana mwenye asili ya Africa Mashariki Barack Obama anaingi Ikulu ya Marekani (WHITE HOUSE) kuwa rais mpya wa 44 wa nchi hiyo
Zaidi ya watu milioni mbili watahudhuria hafla hii ya kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo kubwa Duniani na yenye kuheshimika kupita nchi nyingi na wengine wanathubutu kumuita rais wa nchi hiyo kuwa ni rais wa Dunia
Obama anachukua nafasi ya Rais aliekuwa na jina kubwa Dunaini tena kuliko marais wote hapa Duniani yaani George Bush aliejichukulia sifa kemekm na kulaumiwa na baadhi ya watu kutokana na sera zake za kupambana na magaidi ikiwemo kuivamia kijeshi nchi ya Iraq
Wakati wengine wakiwa mjini Woshington kwenye mjii mkuu wa nchi hiyo kufuatilia kuapishwa kwa OBAMA sisi tutakuwa kwenye luninga zetu nasi tukiwa sambamba kuafuatilia tukio hilo la kuapishwa Obama
Ungana na shirika la Utangazani Tanzania (TBC) ambalo litakuletea matangazo hayo moja kwa moja toka Woshington DC kupitia kituo chake cha luninga cha TBC1
Kila la heli Barack Obama

Robinho atikisa kibiriti


Sasa hili ni noma umesikia Robinho anampango wa kuitema timu yake ya Manchester city aliyojiunga nayo kwa kiwango kikubwa cha pesa eti aliondoka kwenye mazoezi ya timu hiyo bila kuaga
Hiyo imekuja saa chache tu baada ya nduguye Kaka kukataa kujiunga na timu hiyo akitokea timu ya AC Millan ya Italia, kumekuwa na habari za chini ya kapeti zinazosema kijana huyo amerudi kwao Brazil lakini wakuu wa Man city wanashindwa kusema chochote kile juu ya hilo sakata
Hivi kunani hapo Man city? Kaka akatae kujiunga nayo tena kwa mabilioni ya pesa na sasa Robinho anataka kuondoka balaa hilo ndugu yangu ila sisi wana tupo wote yetu ni macho tu pamoja na masikio ya kusikia kinachotokea na kuendelea juu ya huyu bwana mdogo wa Kibrazil

Kaka kuendelea kukipiga AC Millan


Picha kubwa ni Ricardo Kaka juu kulia kwa kaka ni nembo za timu za AC Millan na Machester cty na chini ni makocha wa timu hizo Carlo Ancelotti wa AC Millana kulia na Mark Hughes
Mzee Bosco Leite ambae ni baba mzazi wa Kaka pia ni mshauri mkuu wa mchezaji huyo alisafiri umbali mrefu mno toka Brazil hadi Italia na kumshawishi mwanae kubakia AC Millan

Kaka aitosa Man City


Ama kweli waswahili walinena pesa kwenye mapenzi haifanyi kitu ndio kilichotokea kwa Kiungo mshambuliaji wa timu ya AC Millan ya Italia Mbrazil Ricardo Kaka aliekata kuihama timu hiyo na kujiunga na timu ya Manchester City ya England

Kaka amewashangaza wapenda soka wengi Duniani kwa kukata mapesa mengi ya waarabu waliotaka ajiunge na timu yao kwa kiwango kikubwa cha pesa na angeweka rekodi ya Dunia ya ada ya uhamisho lakini kijana huyo toka Amerika Kusini anakata mabilioni ya waarabu hao na kusema ataendelea kuichezea timu hiyo ya Italia

Sasa swali kwa wchezaji wa kibongo wangeweza kukata hizo pesa kama alivyofanya Kaka? lakini hata mimi ninge.... si unajua tena LIFE yetu ya kibongo sasa jibu unalo

Kila la heli Ricardo Kaka na maamuzi yako yaheshimiwe