Saturday 22 August 2009

Sendeu aula YANGA


Kulia aliezibwa na Camera ndie Louis Sendeu akiwa anava microphone akijianda kumuhoji mchezaji wa mpira wa Kikapu wa Kitanzania anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA Hasheem Thabeet kwenye kipindi cha kila wiki cha Michezo cha kwenye Luninga kinachoitwa MEZA YA MICHEZO kinachorushwa na Television ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayoitwa TBC1 hapo August 16/ 2009.
Hii leo jumamosi 22 August 2009 baada ya kupita wiki moja Louis Sendeu ametangazwa na timu ya ligi kuu Tanzania bara ya YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB (YANGA) kuwa msemaji wa timu hiyo ikiwa siku moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu mpya wa 2009 - 2010.
Yanga ni miongoni mwa timu zilizochelewa kutimiza azimo la Bagamoyo la kila timu za ligi kuu Tanzania bara kuanzi msimu huu wa 2009 - 2010 kuwa na watendaji watu wa kuajiliwa.
Mwingine alieula Yanga ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Yanga Lawrence Mwalusako ambae yeye amekuwa katibu mkuu na mtunza pesa ni Godfrey Mwenje.
Sendeu anakuwa mwandishi na Mtangazaji wa pili toka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa msemaji wa timu ya ligi kuu wa kwanza alikuwa ni Cliford Ndimbo aliechukua cheo kama hicho kwenye timu ya Simba.
Kila la heli mwanahabari mwenzetu Louis Sendeu katika ajira nyingine pamoja na Cliford Ndimbo.

Tuesday 18 August 2009

Hasheem ndani ya TBC









Mchezaji mpira wa kikapu wa Kitanzania Hasheem Thabeet anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA katika timu ya MEMPHIS GRIZZLES ya Tenesse akihojiwa na mwandishi na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Evance Mhando.
Mahojiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za TBC1 Mikocheni Jijini Dar es salaam siku ya jumapili August 16/ 2009 saa nane mchana ambapo Hasheem alienda kutembelea ofisi hizo na kushiriki kwenye kipindi cha wiki cha Michezo kinachoitwa Michezo Yetu kilichoendeshwa na Evance Mhando (Mr Names).
Pamoja na yote Hasheem aliwataka vijana wa Kitanzania kujitahidi kwenye michezo pia na kutilia mkazo swala la Elimu na kutokata tamaa mapema kwenye kila jambo wanalolitaka katika Maisha yao.


Tuesday 11 August 2009

St George yamtosa rasmi Ivo Mapunda


Timu ya ST George ya Ethiopia imesitisha mkataba wake na kipa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Ivo Mapunda aliekuwa akicheza soka la kulipwa kwenye timu hiyo ya Addis Ababa.
Ivo alijiunga na timu hiyo ya ligi kuu nchini humo akitokea timu ya Yanga Africa ya hapa Tanzania mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2008 na kuingia nayo mkataba wa miaka miwili.
Akiongea kwenye kipindi cha michezo cha kila siku cha Radio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inyoitwa TBC Taifa Ivo amesema yeye alirudi nyumbani kwaajili ya mapumziko ila ameshituka kupata habari hizo.
Habari hizo amezipata kwa njia ya Email jioni ya leo jumanne August 11/ 2009 ambayo imetumwa na kocho wa timu hiyo ya ST George Msebia Micho ambae kwa mujibu wa Ivo haina maneno mengi zaidi ya kusema wamestisha mkataba wake.
Akiongea kwenye kipindi hicho cha michezo cha TBC Taifa Ivo amesema kwa sasa atakachofanya yeye ni kufuatilia maslahi yake maana alipojiunga na timu hiyo aliingia nayo mkataba wa miaka miwili na kipindi hicho bado hakijaisha.
Akizungumzia kuhusu kwa sasa ataenda wapi kucheza soka maana hapa Tanzania dirisha la usajili limeshafungwa amesema mameneja wengi wa timu mbalimbali hapa barani Africa wamekuwa wakimsaka na sasa ataanza rasmi kufanya nao mazungumzo.