Monday 30 April 2007

Chuo kikuu cha dare s salaam chawa mingoni mwa vyuo bora duniani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta ALI MOHAMMED SHEIN kesho kutwa anatarajia kufungua mkutano wa wadau wa masuala kuhusiana na tafiti mbalimbali nchini.
Mkutano huo umeandaliwa na ubalozi wa Sweden nchini ambapo utazungumzia namna tafiti mbalimbali zinavyoweza kuleta maendeleo katika jamii nzima nchini Tanzania.
Taarifa kutoka ubalozi wa Sweden imesema mkutano huo utashirikisha wadau mbalimbali nchini zikiwemo taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utafiti na wasomi wa vyuo vikuu.
Nchi zaTanzania na Sweden zimekuwa katika uhusiano wa masuala ya utafiti kwa miaka zaidi ya kumi sasa,katika muda huo uhusiano huo umejikita kwa kutoa elimu na michango kwa vyuo vya elimu ya juu ikiwemo Chuo kikuu cha DAR ES SALAAM.
Kwa hatua hiyo chuo kikuu cha DAR ES SALAAM kupitiano uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili umewezesha chuo hicho kuongoza kwa masuala ya Utafiti kwa vyuo vyote vya elimu ya juu.
Uhusiano huo umewezesha pia Tanzania kupata changamoto ya kuhimiza jamii kujihusisha zaidi na masuala ya utafiti.

Ni vita baina ya wauza mitumba wa Ilala na mnyama Simba

Vita nyingine hii leo ipo mjini Morogoro ambapo wauza mitumba wa katikati ya jiji la Dar es salaam timu ya Ashant United watakapovaana na timu ya Simba pia ya Dar es salaam katika mchezo wa ligi ndogo ya shirikisho la soka hapa nchini TFF
Katika mchezo wao wa kwanza timu hizo mchezo wao haukumalizika hiyo ilikuja baada ya mashabiki wa timu ya Simba kuanzisha vurugu na muamuzi wa mchezo huo akamaliza machezo na katika maamuzi yaliyotolewa na TFF yakaipiga Simba faini ya shiringi 30,0000 pamoja na kunyang`anywa ponti tatu pamoja na kiongozi wao mmoja kufungiwa asijuhusishe na mambo ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja na mchezaji wao hatari Joseph Kaniki kufungiwa asicheze soka michezo sita
Sasa cha kujiuliza nini hili leo kitatokea hii leo mabomu yatapigwa tena?ngoja tusubiri tuone,
Ligi hiyo inaendelea pia katika miji ya Dodoma ambapo timu ya Mtibwa Sugar inacheza na JKT Ruvu na mkoani Arusha wanandugu kutoka mkoa mmoja yaani Moro United wanakipiga na Polisi Morogoro
Simba na Ashant United tayari zimeshafuzu kwa sita bora huku Polisi Dodoma ikiwa inaongoza kituo cha Arusha na JKT Ruvu nao wanaongoza kituo cha Dodoma na Mtibwa Sugar wao wanafuaatia wakiwa wapili katika kituo hicho cha Dodoma

हस्र kwa कम्पुनी या सिमू

Kampuni ya simu Tanzania-TTCL nyanda za juu kusini magharibi imepata hasara ya shilingi Bilioni 2.2 kutokana na wizi wa nyaya za simu na vipuri mbalimbali kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hayo yamesemwa na meneja wa kanda hiyo Bwana SAIDI AMIR wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mjini MBEYA. Amesema maeneo yaliyokumbwa na kuibiwa nyaya hizo na kusababisha wateja wake kukosa mawasiliano ni pamoja na mikoa ya RUVUMA,MBEYA,RUKWA na IRINGA

Tuesday 24 April 2007

Zambia na Libya zakubali kukipiga na Taifa Stars

Wauza mitumba washikwa shati

Baada ya ajari kuongezeka vidhibiti mwendo vyakumbukwa

Chama cha wamiliki wa mabasi nchini-TABOA kimewaagiza wamiliki wa mabasi yote kuhakikisha kuwa mabasi yao yana vidhibiti mwendo vinavyofanyakazi.
Kimesema wakati serikali inafanya jitihada za kutafuta njia mbadala ya kudhibiti mwendo kasi vidhibiti mwendo vilivyopo kwenye mabasi kwa sasa ndio viendelee kutumika.
Agizo hilo limetolewa Mjini DAR ES SALAAM na Mwenyekiti wa Taifa wa TABOA Bwana MOHAMMED ABDULLAH mara baada ya kukutana na Makamanda wa usalama barabarani wa mikoa yote nchini kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha usafirishaji wa abiria.
Katika taarifa yake Bwana ABDULLAH pia amewaagiza abiria wa mabasi hayo kumkemea dereva anayeendesha vibaya ikiwa ni pamoja na kwenda mwendo wa kasi.
Amesema, endapo dereva huyo atakaidi, watoe taarifa ya dereva huyo kwa mmiliki wa basi au kwa polisi wa usalama barabarani.
Mwenyekiti huyo wa chama cha wamiliki wa mabasi nchini amewashauri abiria wote nchini kuwa na utamaduni wa kudai tiketi inayoonyesha nauli anayotozwa, namba ya kiti, sehemu atokayo na aendayo.
Bwana ABDULLAH amesema, endapo kutakuwa na ushirikiano kati ya abiria, wamiliki wa mabasi na askari wa usalama barabarani, usafiri kwa njia ya barabara utaimarishwa na hivyo kupunguza ajali za barabarani.

Kumbe Watanzania wapo makini

Ni muda kidogo umepita toka Ugonjwa wa homa ya bonde la Ufa (RVF)uingie hapa Nchini ambapo watu waliambiwa kuwa wasile nyama ya Ng`ombe na Nyama ya Mbuzi ilikuepuka ugonjwa huo ni kweli watu hawali nyama kabisa
Ni muda kidogo umepita toka walipotoa tangazo hilo na hadi hii leo huwezi kuamini bado wananchi waliowengi hawali kabisa nyama hizo
Ukipita katika mabucha ya Nyama hasa hapa Dar Es Sallam utakuta nyama zikiwa zimewekwa huku wanunuzi ni wachache mno na hata baadhi ya mabucha yamefungwa kwa kukosa wateja wa kununua nyama hizo
Mfakazi mmoja wa bucha moja la Nyama hapa DSM ameuambia mtandao huu kuwa ni hivi sasa kazi ni ngumu mno kwamaana hakuna wateja kabisa wa kununua nyama
Biashara haiendi kabisa yaani wateja hakuna tunaleta nyama hapa Buchani lakini hakuna wa kununu ameeleza mfanyakazi huyo wa hilo bucha
Hongera Watanzania kwa kuwa makini na kuuepuka ugonjwa huo RVF, lakini tusiishie kwenye RVF tu pia tuwemakini hata kwenye ugonjwa hatari wa UKIMWI
Watu wanavyoogopa kula nyama hivi sasa wakihofia kukumbwa na RVF basi tuogope ngono uzembe ilitusipate Ukimwi kwamaana ni hatari zaidi kuliko RVF
Mtu asifanye mapenzi kabla ya ndoa asubiri hadi wakati wake ukifika pale atakapokuwa kwenye ndoa na waliokuwa kwenye ndoa basi waziheshimu ndoa zao wasitoke ovyo kwamaana ni hatari(UKIMWI NI HATARI kuliko RVF sasa tusiogope tu kula nyama hata Ngono tuogope hivyohivyo

Vita nyingine tena bara Ulaya

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa bara Ulaya kati ya Manchester United na AC Millan unachezwa leo usiku katika uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza
kocha wa Man Utd Sir Alex Ferguson anamatumani makubwa ya timu yake kufanya vyema katika mchezo huo ingawa timu yake inakabiliwa na majeruhi kibao ambao wataukosa mchezo wa leo dhidi ya AC Millan ya Italia
wachezaji wa Man Utd ambao wataukosa mchezo wa leo ni Rio Ferdinand Garry Neville, Nemanja Vidic, Mikael Silvestre, Craig Cathcart, Louis Saha, Ji-Sung Park na Kieran Richardson huku kukiwa na wasiwasi kwa mlinzi wa kushoto Patrice Evra kama anakuwa fit basi itamlazimu akae bechi
Sir Ferguson anasema ingawa baadhi ya wachezeji wake mahili wataukosa mchezo huo yeye bado anamatumaini makubwa na kikosi chake kuifunga AC Millan hii leo
Kwa upande wa AC Millan wao hawana matatizo ndani ya kikosi chao ambapo kocha mkuu wa timu hiyo Carlo Ancelotti ameondoka na kikosi kamili kwenda nacho nchini Uingereza kuivaa Manchester United akiwemo mshambuliaji Alberto Gilardino ambae alikosa mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali dhidi ya Buyern Munich ya Ujerumania alipokuwa akitumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano
kocha huko wa AC Millan Carlo Ancelotti amemjumuhisha katika kikosi chake kipa namba moja wa timu hiyo Nelson Dida inagwa anahatihati ya kuukosa mchezo huo kwa kuwa na maumivu ya bega lakini kocha huyo bado anamatumiani makubwa na kipa wake huyo kuwa anaweza kukaa lango(golini)
Manchester United na AC Milla zimewahi kukutana mara sita katika michuanoa hilo ambapo AC Millan imeshinda mara nne na Manchester United imeshinda mara mbili
Refa wa mchezo wa leo ni Kyros Vassaras kutoka nchini Ugiriki,kipute kitaanza saa 21 :45 kwa saa za Africa Mashariki
Michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itaendelea tena hapo kesho kwa mchezo baina ya Chelsea na Liverpool zote za Uingereza

Mnyama Simba azinduka bila Brazil

Michuano ya ligi ndogo ya shirikiso soka hapa Tanzania(TFF) iliyogawanywa katika makundi matatu ilishuhudia hapoa jana mnyama Simba akizunduka na kuitandika timu ya Tanzania Prisons kwa bao 3-0
Magoli yote ya timu ya Simba yalifungwa na kiungo wake mahili ambae ameonyesha kiwango kikubwa cha soka msimu huu Haruna Moshi(Boban) ambae hapo jana alicheza nafasi ya ushambuliaji akiziba nafasi ya mshambuliaji Joseph Kaniki anaetumikia adhabu ya kuwa na kadi nyekundu
Kocha msaidizi wa timu hiyo ambae hivi sasa amebakia peke yake baada ya kocha mkuu wa timu hiyo Mbrzil Nielsen Elias kuitema timu hiyo na kuondoka bila taarifa yeyote ile alisema vijana wake walicheza vizuri hapo jana baada kufuata maelekezo yake aliyoyatoa kabla ya mchezo
katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo matokeo yalikuwa ni sare ya kutofungana hivyo Simba wamejilekebisha na kufanikiwa kupata ushindio huo mkubwa wa magoli 3-0
katika kituo cha Dodoma timu ya Kagera Sugar nayo imezinduka baada ya kuifunga timu ya Pan Africa kutoka Dar Es Salaam(wazee wa mjini) bao 1-0 ,bao hilo peke la Kagera Sugar lilifungwa na Paul Ngwai katika dakika ya tatu ya mchezo
Ligi hiyo ndogo inaendele tena leo katika kituo cha Morogoro kwa mchezo mmoja baina ya Polisi Dodoma ambayo itaumaana na timu ya Ashant United (wauza mitumba wa Ilala) ambayo hapo jumamosi mchezo wao na timu ya Simba ulivunjika baada ya kuzuka vurugu

Monday 23 April 2007

Top 5 za Africa Mashariki kutoka PRT Radio

1 .Missing Ma baby - Amani
2.Si lazima tu do - Nonini
3.Cenderela - Ally Kiba
4.Sinanoma nae - Aman, Jua kali
5.Nakiboona - Juliana
Habari hizi ni kwa mujibu wa Radio Presenter wa PRT -Djaro Arungu
hizi chat ni kwa kila siku za Ijuma pia usikose kusikiliza PRT kila siku .pia usikose kipindi cha Ladha za Africa Mashariki kila siku za Jumatau,Jumatano na Ijuma ,muda ni saa 12:30 jioni hadi saa 2:oo usiku kutoka PRT

Carvalho na Ballack kuikosa Liverpool

Wachezaji wawili mahili wa timu ya Chelsea Michael Ballack na Racrdo Carvalho wapo katika hatihati ya kucheza mchezo wa kesho kutwa wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya timu ya Liverpool
Hadi hivi sasa tayari viongozi wa timu hiyo wanonyesha kukubali kumkosa mlinzi huyo wa kati raia wa Ureno lakini wanajairibu kuangalia nini kifanyike kwa kiungo mahiri kutoka nchini Ujerumani
Michael Ballack aliumia siku ya jumapili kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle ambapo timu hizo zilitoka suluhu ya kutofungana ambapo kiungo huyo alijitinesha enka yake
Pigo hilo la kumkosa Ballack itakuwa ni kumtonesha maumivu kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ambae tayari ameshamkosa kiungo raia wa Ghana ambae ataukosa mchezso huo dhidi ya Liverpool kutokana na kutumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano
katika safu ya ulinzi wa kati Jose Mourinho amebakiwa na nahodha wake tu John Terry hivy kuwa na kazi nyingine ya kutafuta msaidizi wa kumsaidia nahodha huyo ambapo sasa analazimika kumtumia Khalid Boulhrouz au Paulo Ferreira ili kusaidiana na John Terry ilikuweza kuzuia mashambulizi ya Liverpool hapo Jumatano usiku
Ukiondoa tatizo la wachezaji wake kuwamajaruhi sasa kunakingine Mourinho kinawezakumba kwenye mchezo wa marudiano nacho ni kunawachezaji wake wengi wanakadi moja ya njano baadhi yao ni Didier Drogba ,John Terry , John Mikel Obi nk
kama watapata kadi nyingine hapo kesho kutwa basi watakosa mchezo wamarudiano

Gattuso aitaman Man Utd

Kiungo machachali wa timu ya AC Millan ya Italia – Genaro Gattuso amesema kwamba anavutiwa sana na kocha wa timu ya Manchester United - Sir Alex Ferguson pamoja na timu hiyo
Genaro Gattuso anasema kesho atajitahidi kucheza soka la uhakika iliaweze kumshawishi kocha huyo aendeleze mikakati yake ya kumnyakuwa mwisho mwa msimu huu
Kunamawasiliano kati yetu yanaendelea lakini kwasasa ninaangalia nini ninafanya kwaajili ya timu yangu ya AC Millan hasa kwenye mchezo wa kesho wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ULAYA amesema Genaro Gattuso
Genaro Gattuso amekili kwamba ni kweli anandoto ya siku mmoja acheze soka nchini Uingereza na timu anayotaka kuichezea ni Manchester United si nyingine pia a anapendezwa sana na hari ya hewa ya nchi hiyo na kufutiwa na soka linalichezwa kuliko la nchini kwao ITALIA

Ferguson awapamba Ronaldo na Kaka

Kocha wa timu ya Manchester Unieted Sir Alex Ferguson amesema kwamba hapo kesho wachezaji bora zaidi hapa ulimwenguni kwa sasa Cristiano Ronaldo na Ricardo Kaka watakutana kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya
Mchezo huo wa kwanza wa nufu fainali ya michuano hiyo utapigwa nchini UINGEREZA kwenye uwanja wa Old Trafford nyumbani kwa Manchester United
Ninaweza kusema kwamba kwa sasa hakuna wachezaji bora zaidi hapa Duniani kama Cristiano Ronaldo na Ricardo Kaka ameendelea kusema Sir Ferguson, kwamaana Ronaldo amekuwa bora na msaada mkubwa katika msimu huu kwa Manchester United na Kaka hivyo hivyo kwa timu yake ya AC Millan
Kunawachezaji wengine bora kwenye timu zote mbili kama Paolo Maldini lakini hao wawili ni zaidi na ninahakina mchezo huo utakuwa mgumu mno na ninawaambia AC Millan kuwa Manchester United ya msimu huu ni nzuri kupita ya mwaka 2005 waliyoitoa kwenye hatua ya pili na wategeme upinzani wa kweli hakuna wepesi amesema Sir Alex Ferguson

NGOMA BADO NGUMU.




NI BAHATI KWA MAN UTD KWANI MPAKA SASA BADO WANAENDELEA KUONGOZA LIGI, LAITI CHELSEA WANGEPATA USHIDNI KATIKA MECHI YA JANA DHIDI YA NEWCASTLE HII LEO WANGEKUWA WANAZUNGUMZA MENGINE.

LAKINI MECHI BADO ZIPO HUENDA WAKATIMIZA MALENGO YAO YA KUTETE TAJI LA UINGEREZA.