Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta ALI MOHAMMED SHEIN kesho kutwa anatarajia kufungua mkutano wa wadau wa masuala kuhusiana na tafiti mbalimbali nchini.
Mkutano huo umeandaliwa na ubalozi wa Sweden nchini ambapo utazungumzia namna tafiti mbalimbali zinavyoweza kuleta maendeleo katika jamii nzima nchini Tanzania.
Taarifa kutoka ubalozi wa Sweden imesema mkutano huo utashirikisha wadau mbalimbali nchini zikiwemo taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utafiti na wasomi wa vyuo vikuu.
Nchi zaTanzania na Sweden zimekuwa katika uhusiano wa masuala ya utafiti kwa miaka zaidi ya kumi sasa,katika muda huo uhusiano huo umejikita kwa kutoa elimu na michango kwa vyuo vya elimu ya juu ikiwemo Chuo kikuu cha DAR ES SALAAM.
Kwa hatua hiyo chuo kikuu cha DAR ES SALAAM kupitiano uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili umewezesha chuo hicho kuongoza kwa masuala ya Utafiti kwa vyuo vyote vya elimu ya juu.
Uhusiano huo umewezesha pia Tanzania kupata changamoto ya kuhimiza jamii kujihusisha zaidi na masuala ya utafiti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment