Monday, 30 April 2007

Ni vita baina ya wauza mitumba wa Ilala na mnyama Simba

Vita nyingine hii leo ipo mjini Morogoro ambapo wauza mitumba wa katikati ya jiji la Dar es salaam timu ya Ashant United watakapovaana na timu ya Simba pia ya Dar es salaam katika mchezo wa ligi ndogo ya shirikisho la soka hapa nchini TFF
Katika mchezo wao wa kwanza timu hizo mchezo wao haukumalizika hiyo ilikuja baada ya mashabiki wa timu ya Simba kuanzisha vurugu na muamuzi wa mchezo huo akamaliza machezo na katika maamuzi yaliyotolewa na TFF yakaipiga Simba faini ya shiringi 30,0000 pamoja na kunyang`anywa ponti tatu pamoja na kiongozi wao mmoja kufungiwa asijuhusishe na mambo ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja na mchezaji wao hatari Joseph Kaniki kufungiwa asicheze soka michezo sita
Sasa cha kujiuliza nini hili leo kitatokea hii leo mabomu yatapigwa tena?ngoja tusubiri tuone,
Ligi hiyo inaendelea pia katika miji ya Dodoma ambapo timu ya Mtibwa Sugar inacheza na JKT Ruvu na mkoani Arusha wanandugu kutoka mkoa mmoja yaani Moro United wanakipiga na Polisi Morogoro
Simba na Ashant United tayari zimeshafuzu kwa sita bora huku Polisi Dodoma ikiwa inaongoza kituo cha Arusha na JKT Ruvu nao wanaongoza kituo cha Dodoma na Mtibwa Sugar wao wanafuaatia wakiwa wapili katika kituo hicho cha Dodoma

No comments: