Tuesday, 24 April 2007

Vita nyingine tena bara Ulaya

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa bara Ulaya kati ya Manchester United na AC Millan unachezwa leo usiku katika uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza
kocha wa Man Utd Sir Alex Ferguson anamatumani makubwa ya timu yake kufanya vyema katika mchezo huo ingawa timu yake inakabiliwa na majeruhi kibao ambao wataukosa mchezo wa leo dhidi ya AC Millan ya Italia
wachezaji wa Man Utd ambao wataukosa mchezo wa leo ni Rio Ferdinand Garry Neville, Nemanja Vidic, Mikael Silvestre, Craig Cathcart, Louis Saha, Ji-Sung Park na Kieran Richardson huku kukiwa na wasiwasi kwa mlinzi wa kushoto Patrice Evra kama anakuwa fit basi itamlazimu akae bechi
Sir Ferguson anasema ingawa baadhi ya wachezeji wake mahili wataukosa mchezo huo yeye bado anamatumaini makubwa na kikosi chake kuifunga AC Millan hii leo
Kwa upande wa AC Millan wao hawana matatizo ndani ya kikosi chao ambapo kocha mkuu wa timu hiyo Carlo Ancelotti ameondoka na kikosi kamili kwenda nacho nchini Uingereza kuivaa Manchester United akiwemo mshambuliaji Alberto Gilardino ambae alikosa mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali dhidi ya Buyern Munich ya Ujerumania alipokuwa akitumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano
kocha huko wa AC Millan Carlo Ancelotti amemjumuhisha katika kikosi chake kipa namba moja wa timu hiyo Nelson Dida inagwa anahatihati ya kuukosa mchezo huo kwa kuwa na maumivu ya bega lakini kocha huyo bado anamatumiani makubwa na kipa wake huyo kuwa anaweza kukaa lango(golini)
Manchester United na AC Milla zimewahi kukutana mara sita katika michuanoa hilo ambapo AC Millan imeshinda mara nne na Manchester United imeshinda mara mbili
Refa wa mchezo wa leo ni Kyros Vassaras kutoka nchini Ugiriki,kipute kitaanza saa 21 :45 kwa saa za Africa Mashariki
Michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itaendelea tena hapo kesho kwa mchezo baina ya Chelsea na Liverpool zote za Uingereza

No comments: