Tuesday 22 December 2009

Kesho ni vita ya Wakenya kwenye Shamba la bibi

Makocha wa timu za SOFAPAKA NA TUSKER zote kutoka Kenya wametambiana kushinda katika mchezo wao wa NUSU FAINALI wa michuano ya kombe la TUSKER Mchezo utakaofanyika hapo kesho katika uwanja wa UHURU Jijini DSM.
Katika mchezo huo wa nusu fainali timu itakayoshinda itakutana katika fainali mshindi wa mchezo kati ya SIMBA au YANGA zinazotarajia kucheza alhamisi wiki hii.
Kwa upande wake kocha wa timu ya TUSKER James Nandwa amesema makosa yaliofanyika katika mchezo na YANGA hayatajirudia tena kwani wachezaji wake wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo na wamejinda kushinda.Kocha wa mabingwa wa Kenya msimu huu timu ya Sofapaka Robert Matano amesema msimu huu Tusker ni wao na hapo kesho wanaenda kushinda tu mchezo huo sio kingine.

Nyota Simba hati hati kuikosa Yanga

Bado kichwa kinawauma wakuu wa bechi la ufundi la Simba kutokana na wachezaji wake mahiri wanne kuwa majeruhi na kutia hofu kama wanaweza kucheza mchezo wa nusu fainali wa kombe la TUSKER dhidi ya watani wao wa jadi wa soka la Tanzania Yanga.
Mchezo huo utachezwa siku ya Alhamis siku moja kabla ya sikuku ya X-masss kwenye dimba la Taifa (Shamba la Babu) na wachezaji ambao ni majeruhi hadi leo ni pamoja na nahodha Nico Nyagawa,Haruna Moshi Boban,Emmanuel Okwi na kiungo Uhuru Selemani ambae tayari imeshathitika kuwa hatocheza mchezo huo.
Meneja wa timu hiyo ya Simba Innocent Njovu amesema bado hawajui chochote kama wachezaji hao watacheza mchezo huo siku ya Alhamis au la ila bado wanaendelea na matibabu.
Njovu amesema mustakabali wa swala hilo litajulikanika hapo kesho kama wachezaji hao watacheza mchezo dhidi ya Yanga au hawatocheza.

Monday 21 December 2009

Yanga na Simba kukipiga Taifa Mpya nusu fainali ya Tusker

Shirikisho la soka hapa nchini (TFF) kwa kushirikiana na waandaaji wa michuano ya kombe la Tusker wamesema mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano hiyo baina ya watani wa jadi wa soka la Tanzania Yanga na Simba utapigwa kwenye dimba la Taifa (Shamba la babu).
Pamoja na kusema hivyo TFF imeweka wazi viingilio vya mchezo huo ambayo hazina tofauti na michezo mingine ya timu hizo mbili zinapokutana kwenye michuano mbali mbali.
Kiingilio cha juu siku hiyo ni elfu 40 huku kiingilioa cha chini kikiwa ni elfu 5.
Mchezo huo wawatani wa jadi utapigwa siku ya Alhamis Desemba 24 siku moja kabla ya sikuku ya xmass, mchezo huo utatanguliwa na mchezo baina ya wakenya watupu timu za Sofabaka na Tusker.
Msemaji wa TFF- Florian Kaijage amesema kuwa wao walishindwa kusema mapema kuwa mchezo huo utachezwa kwenye dimba la Taifa kwasababu uwanja huo unamilikiwa na Serikali lakini sasa kila kitu kipo safi.

PST na TPBO watofautiana kuhusu mpinzani sahihi wa Cheka


Chama cha ngumi za kulipwa nchini (TPBO) kimekanusha taarifa za kuwepo kwa dhuluma katika pambano la ngumi za kulipwa ambapo bondia FRANCIS CHEKA alibadilishiwa mpinzani siku moja kabla ya pambano.
Utata mkubwa juu ya pambano hilo uliibuka mara baada ya kuwepo kwa taarifa za kutowasili kwa bondia huyo hali iliyowashitua wapenzi wengi wa masumbwi ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa pambano hilo.
Hata hivyo pambano hilo lilifanyika ambapo FRANCIS CHEKA alipewa mpinzani toka Brazil na kumchakaza mpinzani wake huyo anaeitwa ISAACK TARAVES kwa KNOCK OUT katika raundi ya pili na kufanikiwa kutetea taji lake la IBO na WBC.
Rais wa TPBO YASSIN ABDALAH amesema kuwa uamuzi wa kubadilisha bondia ulitokana na kuchelewa kwa hati ya kusafiria ya bondia HENRIQ ARECO ambaye awali alitakiwa kupigana na Cheka.
Kauli hiyo inatofautiana na ya Rais wa shirikisho lingene la masumbwi ya kulipwa hapa nchini PST – Emmanuel Mlundwa ambae aliwambia mashabiki siku ya pambano kuwa bondia huyo hakua kwasababu ni mzee, sasa tuamini la nani … ni mzee au alikosa hati ya kusafiria…..

Wadau wa masumbwi wanadai kuwa huo ni ufisadi sasa mimi siju …

Friday 18 December 2009

Hayo ndio mafunzo ya FIFA

Wapiga picha wakiwa na mwalimu wao Erick toka Ufaransa baada ya kumalizika mpira.
Sawa kaka leteni picha zenye kiwango ... hayo ndio mambo ya FIFA ... huyo ni mpira picha wa TBC1 Samwel Mshana akiwa na mwenzie Nicholaus Mbaga.

aaahhh kaka Jacob Mani lete vitu..... unatisha
Wapiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakipiga picha wakati wa mafuzo ya vitendo ya kupiga picha za mpira wakati timu ya Simba ikicheza na timu ya SOFA PAKA ya Kenya kwenye michuano ya kombe la Tusker.
Wapiga picha hao pamoja na watangazaji wa mpira wa Radio na TV na wasimamizi wa Matangazo toka TBC na Chanel Ten wanapata mafuzo ya wiki moja yaliyoandaliwa na shirikisho la la soka Dunia (FIFA) jinsi ya kupiga picha na kutanga mpira pamoja na jinsi ya kusimamia na kuendesha matangazo ya moja kwa moja yaan LIVE ya mpira wa miguu.


Saturday 22 August 2009

Sendeu aula YANGA


Kulia aliezibwa na Camera ndie Louis Sendeu akiwa anava microphone akijianda kumuhoji mchezaji wa mpira wa Kikapu wa Kitanzania anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA Hasheem Thabeet kwenye kipindi cha kila wiki cha Michezo cha kwenye Luninga kinachoitwa MEZA YA MICHEZO kinachorushwa na Television ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayoitwa TBC1 hapo August 16/ 2009.
Hii leo jumamosi 22 August 2009 baada ya kupita wiki moja Louis Sendeu ametangazwa na timu ya ligi kuu Tanzania bara ya YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB (YANGA) kuwa msemaji wa timu hiyo ikiwa siku moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu mpya wa 2009 - 2010.
Yanga ni miongoni mwa timu zilizochelewa kutimiza azimo la Bagamoyo la kila timu za ligi kuu Tanzania bara kuanzi msimu huu wa 2009 - 2010 kuwa na watendaji watu wa kuajiliwa.
Mwingine alieula Yanga ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo ya Yanga Lawrence Mwalusako ambae yeye amekuwa katibu mkuu na mtunza pesa ni Godfrey Mwenje.
Sendeu anakuwa mwandishi na Mtangazaji wa pili toka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa msemaji wa timu ya ligi kuu wa kwanza alikuwa ni Cliford Ndimbo aliechukua cheo kama hicho kwenye timu ya Simba.
Kila la heli mwanahabari mwenzetu Louis Sendeu katika ajira nyingine pamoja na Cliford Ndimbo.

Tuesday 18 August 2009

Hasheem ndani ya TBC









Mchezaji mpira wa kikapu wa Kitanzania Hasheem Thabeet anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA katika timu ya MEMPHIS GRIZZLES ya Tenesse akihojiwa na mwandishi na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Evance Mhando.
Mahojiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za TBC1 Mikocheni Jijini Dar es salaam siku ya jumapili August 16/ 2009 saa nane mchana ambapo Hasheem alienda kutembelea ofisi hizo na kushiriki kwenye kipindi cha wiki cha Michezo kinachoitwa Michezo Yetu kilichoendeshwa na Evance Mhando (Mr Names).
Pamoja na yote Hasheem aliwataka vijana wa Kitanzania kujitahidi kwenye michezo pia na kutilia mkazo swala la Elimu na kutokata tamaa mapema kwenye kila jambo wanalolitaka katika Maisha yao.


Tuesday 11 August 2009

St George yamtosa rasmi Ivo Mapunda


Timu ya ST George ya Ethiopia imesitisha mkataba wake na kipa wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Ivo Mapunda aliekuwa akicheza soka la kulipwa kwenye timu hiyo ya Addis Ababa.
Ivo alijiunga na timu hiyo ya ligi kuu nchini humo akitokea timu ya Yanga Africa ya hapa Tanzania mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2008 na kuingia nayo mkataba wa miaka miwili.
Akiongea kwenye kipindi cha michezo cha kila siku cha Radio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inyoitwa TBC Taifa Ivo amesema yeye alirudi nyumbani kwaajili ya mapumziko ila ameshituka kupata habari hizo.
Habari hizo amezipata kwa njia ya Email jioni ya leo jumanne August 11/ 2009 ambayo imetumwa na kocho wa timu hiyo ya ST George Msebia Micho ambae kwa mujibu wa Ivo haina maneno mengi zaidi ya kusema wamestisha mkataba wake.
Akiongea kwenye kipindi hicho cha michezo cha TBC Taifa Ivo amesema kwa sasa atakachofanya yeye ni kufuatilia maslahi yake maana alipojiunga na timu hiyo aliingia nayo mkataba wa miaka miwili na kipindi hicho bado hakijaisha.
Akizungumzia kuhusu kwa sasa ataenda wapi kucheza soka maana hapa Tanzania dirisha la usajili limeshafungwa amesema mameneja wengi wa timu mbalimbali hapa barani Africa wamekuwa wakimsaka na sasa ataanza rasmi kufanya nao mazungumzo.

Friday 31 July 2009

Mkuu wa makapela apata jiko .... wengine vipi ....


Mwandishi wa michezo wa magazeti ya The Guardian ltd Jimmy Charles (kulia) akimvisha pete mkewe Ruth Lugoe ambaye alifunga nae ndoa katika kanisa katoliki la Boko Dar es salaam jana

Wednesday 18 February 2009

Maembe anatisha


Vitali Maembe ni mwanamuziki wa Kitanzania anaeimba kwa hisia sana na sasa naambiwa hayupo hapa nchini ameenda nchini Norway ambako anafanya kazi ya kufundisha Muziki na lugha ya Kiswahili
Aliwika sana katika wimbo wake wa Sumu ya Teja lakini pia ana nyimbo nyingi kama vile Uwanja wa Taifa ambao aliuimba maalum kwa uwanja mpya wa taifa uliokabidhiwa hivi karibuni kwaTanzania na serikali ya China na zingine ni pamoja na Kiombwe, Africa shilingi tano
Mungu akubariki huko uliko kwa kila ulifanyalo

Huyu ndie alietunga Mjomba

Wengi hawajua kama Irine Sanga ndie mtunzi wa wimba uliowika kupita kiasi wa MJOMBA ulioimbwa na Mrisho Mpoto .... watu wanaupenda sana wimbo huo kutokana na ujumba mzito uliopo ndani yake .... sasa mama tunasubiri kitu kingine kikali zaidi ya kile maana unatisha

Sunday 15 February 2009

Mourinho ataka kurudi Chelsea



Kocha wa zamani wa timu ya Chelsea na kocha wa sasa wa timu ya INTER MILLAN ya Itali Jose Mourinho anasema yu radhi kurudi kwenye timu yake hiyo ya zamani ya Chelsea ili kuifundisha tena kwa mara ya pili

Mourinho amesema kama ukimuuliza unaweza kurudi tena siku moja Kuifundisha Chelsea jibu lake litakuwa ndio kwamaana anaipenda sana timu hiyo

Huu ndio uwanja wa Taifa


Baada ya kumalizwa kujengwa uwanja huu uliitwa uwanja mpya wa taifa baade ukaitwa uwanja mkuu wa taifa na sasa umepewa jina rasmi na kuitwa Uwanja wa Taifa
na ule uwanja wa taifa wa zamani unaitwa uwanja wa Uhuru

Shamba la bibi la badilishwa jina


Huu ni ulikuwa ukiitwa uwanja wa Taifa na baadae utakitwa uwnja wa taifa wa zamani na sasa umebadilishwa jina na unaitwa uwanja wa UHURU
Kaulia ya kubadilishwa jina imetolewa na waziri wa Habri utamaduni na Michezo Mh George Mkuchika