Tuesday 22 December 2009

Kesho ni vita ya Wakenya kwenye Shamba la bibi

Makocha wa timu za SOFAPAKA NA TUSKER zote kutoka Kenya wametambiana kushinda katika mchezo wao wa NUSU FAINALI wa michuano ya kombe la TUSKER Mchezo utakaofanyika hapo kesho katika uwanja wa UHURU Jijini DSM.
Katika mchezo huo wa nusu fainali timu itakayoshinda itakutana katika fainali mshindi wa mchezo kati ya SIMBA au YANGA zinazotarajia kucheza alhamisi wiki hii.
Kwa upande wake kocha wa timu ya TUSKER James Nandwa amesema makosa yaliofanyika katika mchezo na YANGA hayatajirudia tena kwani wachezaji wake wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo na wamejinda kushinda.Kocha wa mabingwa wa Kenya msimu huu timu ya Sofapaka Robert Matano amesema msimu huu Tusker ni wao na hapo kesho wanaenda kushinda tu mchezo huo sio kingine.

Nyota Simba hati hati kuikosa Yanga

Bado kichwa kinawauma wakuu wa bechi la ufundi la Simba kutokana na wachezaji wake mahiri wanne kuwa majeruhi na kutia hofu kama wanaweza kucheza mchezo wa nusu fainali wa kombe la TUSKER dhidi ya watani wao wa jadi wa soka la Tanzania Yanga.
Mchezo huo utachezwa siku ya Alhamis siku moja kabla ya sikuku ya X-masss kwenye dimba la Taifa (Shamba la Babu) na wachezaji ambao ni majeruhi hadi leo ni pamoja na nahodha Nico Nyagawa,Haruna Moshi Boban,Emmanuel Okwi na kiungo Uhuru Selemani ambae tayari imeshathitika kuwa hatocheza mchezo huo.
Meneja wa timu hiyo ya Simba Innocent Njovu amesema bado hawajui chochote kama wachezaji hao watacheza mchezo huo siku ya Alhamis au la ila bado wanaendelea na matibabu.
Njovu amesema mustakabali wa swala hilo litajulikanika hapo kesho kama wachezaji hao watacheza mchezo dhidi ya Yanga au hawatocheza.

Monday 21 December 2009

Yanga na Simba kukipiga Taifa Mpya nusu fainali ya Tusker

Shirikisho la soka hapa nchini (TFF) kwa kushirikiana na waandaaji wa michuano ya kombe la Tusker wamesema mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano hiyo baina ya watani wa jadi wa soka la Tanzania Yanga na Simba utapigwa kwenye dimba la Taifa (Shamba la babu).
Pamoja na kusema hivyo TFF imeweka wazi viingilio vya mchezo huo ambayo hazina tofauti na michezo mingine ya timu hizo mbili zinapokutana kwenye michuano mbali mbali.
Kiingilio cha juu siku hiyo ni elfu 40 huku kiingilioa cha chini kikiwa ni elfu 5.
Mchezo huo wawatani wa jadi utapigwa siku ya Alhamis Desemba 24 siku moja kabla ya sikuku ya xmass, mchezo huo utatanguliwa na mchezo baina ya wakenya watupu timu za Sofabaka na Tusker.
Msemaji wa TFF- Florian Kaijage amesema kuwa wao walishindwa kusema mapema kuwa mchezo huo utachezwa kwenye dimba la Taifa kwasababu uwanja huo unamilikiwa na Serikali lakini sasa kila kitu kipo safi.

PST na TPBO watofautiana kuhusu mpinzani sahihi wa Cheka


Chama cha ngumi za kulipwa nchini (TPBO) kimekanusha taarifa za kuwepo kwa dhuluma katika pambano la ngumi za kulipwa ambapo bondia FRANCIS CHEKA alibadilishiwa mpinzani siku moja kabla ya pambano.
Utata mkubwa juu ya pambano hilo uliibuka mara baada ya kuwepo kwa taarifa za kutowasili kwa bondia huyo hali iliyowashitua wapenzi wengi wa masumbwi ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa pambano hilo.
Hata hivyo pambano hilo lilifanyika ambapo FRANCIS CHEKA alipewa mpinzani toka Brazil na kumchakaza mpinzani wake huyo anaeitwa ISAACK TARAVES kwa KNOCK OUT katika raundi ya pili na kufanikiwa kutetea taji lake la IBO na WBC.
Rais wa TPBO YASSIN ABDALAH amesema kuwa uamuzi wa kubadilisha bondia ulitokana na kuchelewa kwa hati ya kusafiria ya bondia HENRIQ ARECO ambaye awali alitakiwa kupigana na Cheka.
Kauli hiyo inatofautiana na ya Rais wa shirikisho lingene la masumbwi ya kulipwa hapa nchini PST – Emmanuel Mlundwa ambae aliwambia mashabiki siku ya pambano kuwa bondia huyo hakua kwasababu ni mzee, sasa tuamini la nani … ni mzee au alikosa hati ya kusafiria…..

Wadau wa masumbwi wanadai kuwa huo ni ufisadi sasa mimi siju …

Friday 18 December 2009

Hayo ndio mafunzo ya FIFA

Wapiga picha wakiwa na mwalimu wao Erick toka Ufaransa baada ya kumalizika mpira.
Sawa kaka leteni picha zenye kiwango ... hayo ndio mambo ya FIFA ... huyo ni mpira picha wa TBC1 Samwel Mshana akiwa na mwenzie Nicholaus Mbaga.

aaahhh kaka Jacob Mani lete vitu..... unatisha
Wapiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakipiga picha wakati wa mafuzo ya vitendo ya kupiga picha za mpira wakati timu ya Simba ikicheza na timu ya SOFA PAKA ya Kenya kwenye michuano ya kombe la Tusker.
Wapiga picha hao pamoja na watangazaji wa mpira wa Radio na TV na wasimamizi wa Matangazo toka TBC na Chanel Ten wanapata mafuzo ya wiki moja yaliyoandaliwa na shirikisho la la soka Dunia (FIFA) jinsi ya kupiga picha na kutanga mpira pamoja na jinsi ya kusimamia na kuendesha matangazo ya moja kwa moja yaan LIVE ya mpira wa miguu.