Tuesday 22 December 2009

Nyota Simba hati hati kuikosa Yanga

Bado kichwa kinawauma wakuu wa bechi la ufundi la Simba kutokana na wachezaji wake mahiri wanne kuwa majeruhi na kutia hofu kama wanaweza kucheza mchezo wa nusu fainali wa kombe la TUSKER dhidi ya watani wao wa jadi wa soka la Tanzania Yanga.
Mchezo huo utachezwa siku ya Alhamis siku moja kabla ya sikuku ya X-masss kwenye dimba la Taifa (Shamba la Babu) na wachezaji ambao ni majeruhi hadi leo ni pamoja na nahodha Nico Nyagawa,Haruna Moshi Boban,Emmanuel Okwi na kiungo Uhuru Selemani ambae tayari imeshathitika kuwa hatocheza mchezo huo.
Meneja wa timu hiyo ya Simba Innocent Njovu amesema bado hawajui chochote kama wachezaji hao watacheza mchezo huo siku ya Alhamis au la ila bado wanaendelea na matibabu.
Njovu amesema mustakabali wa swala hilo litajulikanika hapo kesho kama wachezaji hao watacheza mchezo dhidi ya Yanga au hawatocheza.

No comments: