Tuesday, 9 October 2007

Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea kesho katika viwanja mbalimbali hapa nchini Tanzania huku mchezo mkali ukiwa ni baina ya wanaongoza ligi hiyo Tanzania Prisons ya Jijini Mbeya wanataocheza na mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Simba kutoka katika mjii mkuu wa kibiashara wa Silvio BerlusconiTanzania unaoitwa Dar es salaama
Hadi sasa timu ya Tanzania [Prisons ndio inayaoongoza ligi hii ya Tanzania bara ikiwa na pointi 15 ambapo imeshinda michezo yake yote mitano ambayo minne imecheza nyumbani kwenye uwanja wa Sokoine na mmoja dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani ikishinda ugenini
Simba wao wameanza ligi hii kwa mwendo wa kusuasua ambapo hadi sasa wanapointi sita huku wakishinda mchezo moja dhidi ya Mtibwa sugar jumapili iliyopita na kutoka sare mara matau na kufungwa mchezo moja dhidi ya Coast Union ya Tanga ambayo nayo junmapili iliyopita ilipoke kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Prisons
Ratiba ya michezo mingine ya hapo kesho na kesho kutwa Alhamis ni kama ifuatavyo hapo chini pamoja na majina ya waamuzi watakaochezesha michezo hiyo kama ilivyotolewa na shirikisho la soka Tanzania ( TFF)
MZUNGUKO WA 6
10-Oct-07
36
Jkt Ruvu vs Coastal Union
Arusha
M
Allanus Lwena
Mwanza




MM
Wilson Elisha
Mwanza




MM
Justine Shija
Mwanza




MA
Samwel Mpenzu
Arusha







10-Oct-07
37
Tz Prisons vs Simba
Mbeya
M
Damian Mabena
Tanga




MM
Rashid Lwena
Ruvuma




MM
Yusuf Sekile
Ruvuma




MA
Andongwise Panja
Mbeya







10-Oct-07
38
Polisi Dodoma vs Polisi Moro
Dodoma
M
Othman Kazi
D'salaam




MM
Abdallah Selega
D'salaam




MM
Said Chande
D'salaam




MA
Charles Ndagala
Dodoma







10-Oct-07
39
Moro United vs Mtibwa Sugar
Morogoro
M
David Paul
Mtwara




MM
Frank Mwenda
Lindi




MM
Idd Maganga
D'salaam




MA
Athuman Lazi
Morogoro







10-Oct-07
40
Manyema vs Pan African
Tanga
M
Oden Mbaga
D'salaam




MM
Zahara Mohamed
D'salaam




MM
Godrey Tumaini
D'salaam




MA
Rashidi Gogola
Tanga







11-Oct-07
41
Yanga vs Toto African
Morogoro
M
Vicent Ndunguru
Ruvuma




MM
Ismail Mshana
Dodoma




MM
Riziki Majala
Pwani




MA
Jessey Erasmo
Morogoro







11-Oct-07
42
Ashanti United vs Kagera Sugar
Moshi
M
Ibrahim Kidiwa
Tanga




MM
Gamaliel Makange
Tanga




MM
Yahaya Ally
Mara




MA
Beda Lymo
K'njaro

Tuesday, 1 May 2007

SIMBA WASHINDWA KULIPA HOSTEL MORO

Ama kwa hakina mpenzi wa soka huwezi kuamini timu ya Simba imeshindwa kulipa kiasi cha shilingi 140000 za kitanzania kwa ajiri ya kulipia Hostel waliyokuwa wakikaa kwa kipindi cha wiki mbili za mashindano ya ligi ndogo ya TFF
Habari kutoka Morogoro zinasema kwamba wachezaji wa timu hiyo waliluhusiwa kuondoka kwenye Hostel za chuo kikuu cha Waislamu mkoani humo lakini gari la kingozi mmoja wa timu hiyo ya Simba aina ya Toyota Prado namba T276ABX limezuhiliwa hadi pale viongozi wa timu hiyo ya Simba watakapolipa deni hilo
Mmoja wa viongozi wa Hostel hiyo ameuammbia mtandao huu kuwa kwa kipindi cha wiki zote mbili walizokaa pale ni wiki moja tu viongozi wa timu hiyo walilipa kodi lakini wiki nyingine moja hawakulipa kodi na walitaka kuwazuia na wachezaji wa timu hiyo wasiondoke lakini wamemua kuwaachia na kulizuia gari hilo hadi pale watakapopata pessa zao
Katika Hostel hiyo Simba walikuwa wakipata huduma mbalimbali kama vile chakula na uwanja wa kufanyia mazoezi na kila kitu walitakiwa kukilipia lakini wao hawakulipa na viongozi wa Hostel hiyo waliwaamini sana viongozi wa timu hiyo lakini hivi sasa uaminifu wao umekwisha
Hapo jana timu ya Simba walicheza mchezo wao wa mwisho wa michuano hiyo ya ligi ndogo dhidi ya Ashant United na kupokea kipigo cha bao 2-0 hivvo kumaliza michuno hiyo wakiwa wa pili nyuma ya wauza mitumba hao kutoka mitaa ya ILALA hapa Dar es salaam

John Terry atamani kuifundisha Cheslea

Nahodha wa timu ya Chelsea John Terry amesema anataka baada ya kustafu kuichezea timu hiyo basi awe kocha wa timu hiyo
John Terry ameliambia shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kuwa anataka siku moja awe kocha wa timu ya Chelsea pale atakapo sitafu kucheza soka
Ameendelea kueleza kwamba pale alipokuwa akizungumza na viongozi wa timu hiyo kuhusu mkataba wake aliwambia wampe makataba wa miaka tisa na baada ya hapoa basi awe kocha wa timu hiyo
Sina hamu kabisa ya kuhama Chelsea kwamaana ninataka nipate mafunzo ya ukocha na baadae nije niifundisha timu hiii ninayoipenda ameeleza John Terry

Nani mtemi hii leo baina ya Liverpool na Chelsea

Ni mara nyingine tena timu mbili za nchini Uingereza za Liverpool na Chelsea zinamumaana kwenye mchezo wa marudianao wa ligi ya mabingwa barani Ulaya
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa Chelsea mabilione hao walifanikiwa kuifunga Liverpool bao 1- 0,bao lilofungwa na kiungo mchambuliaji Joe Cole
Mchezo wa leo unapigwa kwenye uwanjwa wa Anfield nyumbani kwa Liverpool huku wenyeji hao wakiwa na matumaini makubwa kurudi yake walioyafanya mwaka 2005 ambapo walifanikiwa kuitoa Chelsea kwenye michuno hiyo baada ya kuinyuka baoa 1-0,bao lilotiwa kimiani na Luis Gacia
Hii leo Chelsea itaingia dimbani bila la kiungo wake rai wa Ujerumani Michael Ballack aliemajeruhi na mlinzi wa kati Ricardo Carvslho ambae nae ni majeruhi hinyo kumfanya kocha wa Chelsea Jose Mourinho kuumia kichwa
Katika hatua hiyo Mourinho atalazimika kumtumia kiungo wa Ghana Michael Essien kama m linzi wa kati akishirikia na John Terry ilikuweza kulinda ngome ya timu hiyo pamoja na kulinda ushindi wao wa goli moja walioupata nyumbani kwao
Kunauwezekana pia mshambuliaji hatari wa timu ya Chelsea raia wa Ukrain Andriy Shevchenko akaukosa mchezo wa leo kutokana na maumivu ya misuli hivyo kuzi kumuumiza Jose Mourinho
Kwa upande wa Liverpool wao hawana amatatizo kabisa kwamaana kikosi chao chote ni kizima na hakina matatizo yeyote yake
Na kocha wa Liverpool Rafael Benitez amejigamba kuwa lazima waitoe timu hiyo kwamaana wamejianda kikamilifu na wanahamu tena ya kucheza fainali ya michuno hiyo kama walivyofanya mwaka 2005

Wauza mitumba wamuua mnyama Simba

Wauza mitumba wa Ilala timu ya Ashant hapo jana walizihilisha kuwa wao ni mwamba kwa timu ya Simba baada ya kuinyuka timu hiyo bao 2-0 kwenye mchezo wa ligi ndogo ya TFF
Uzembe uliofanywa na mlinzi wa kati timu ya Simba Said Kokoo ulimpa nafasi mshambuliaji Mussa Kipao kuipatia timu yake ya Ashant United bao la kwanza katika dakika ya 18 na kuifanya timu yake iwe mbele kwa bao hilo moja hadi mapumziko
Ashant United walikomelea msumari wa moto na wa mwisho kwenye jeneza la timu ya Simba katika dakika ya 54 kupitia kwa mshambuliaji wake Patrick Mrope aliemzidi mbio mlinzi wa Simba Nurdin Bakari
Kwa matokeo hayo Ashant United imezihilisha uwamba wake kwa timu hiyo ya msimbazi kwamaana katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo haukumalizika baada ya mashabiki wa timu ya Simba kuanzisha vurugu na TFF ikaamuru kuipa Ashant United pont tatu na magoli mawili
Pia kwa matokeo hayo Ashant United imefanikiwa kuongoza kituo cha Morogoro kwa kuwa na point 13 na kufuatiwa na timu ya Simba yenye point 10
Timu hizo zote mbili zimefanikiwa kuingia hatua ya sita bora ambapo hivi sasa zinasubiria timu zingine nne kutoka katika vitua vya Arusha na Dodoma

Monday, 30 April 2007

Chuo kikuu cha dare s salaam chawa mingoni mwa vyuo bora duniani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta ALI MOHAMMED SHEIN kesho kutwa anatarajia kufungua mkutano wa wadau wa masuala kuhusiana na tafiti mbalimbali nchini.
Mkutano huo umeandaliwa na ubalozi wa Sweden nchini ambapo utazungumzia namna tafiti mbalimbali zinavyoweza kuleta maendeleo katika jamii nzima nchini Tanzania.
Taarifa kutoka ubalozi wa Sweden imesema mkutano huo utashirikisha wadau mbalimbali nchini zikiwemo taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utafiti na wasomi wa vyuo vikuu.
Nchi zaTanzania na Sweden zimekuwa katika uhusiano wa masuala ya utafiti kwa miaka zaidi ya kumi sasa,katika muda huo uhusiano huo umejikita kwa kutoa elimu na michango kwa vyuo vya elimu ya juu ikiwemo Chuo kikuu cha DAR ES SALAAM.
Kwa hatua hiyo chuo kikuu cha DAR ES SALAAM kupitiano uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili umewezesha chuo hicho kuongoza kwa masuala ya Utafiti kwa vyuo vyote vya elimu ya juu.
Uhusiano huo umewezesha pia Tanzania kupata changamoto ya kuhimiza jamii kujihusisha zaidi na masuala ya utafiti.

Ni vita baina ya wauza mitumba wa Ilala na mnyama Simba

Vita nyingine hii leo ipo mjini Morogoro ambapo wauza mitumba wa katikati ya jiji la Dar es salaam timu ya Ashant United watakapovaana na timu ya Simba pia ya Dar es salaam katika mchezo wa ligi ndogo ya shirikisho la soka hapa nchini TFF
Katika mchezo wao wa kwanza timu hizo mchezo wao haukumalizika hiyo ilikuja baada ya mashabiki wa timu ya Simba kuanzisha vurugu na muamuzi wa mchezo huo akamaliza machezo na katika maamuzi yaliyotolewa na TFF yakaipiga Simba faini ya shiringi 30,0000 pamoja na kunyang`anywa ponti tatu pamoja na kiongozi wao mmoja kufungiwa asijuhusishe na mambo ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja na mchezaji wao hatari Joseph Kaniki kufungiwa asicheze soka michezo sita
Sasa cha kujiuliza nini hili leo kitatokea hii leo mabomu yatapigwa tena?ngoja tusubiri tuone,
Ligi hiyo inaendelea pia katika miji ya Dodoma ambapo timu ya Mtibwa Sugar inacheza na JKT Ruvu na mkoani Arusha wanandugu kutoka mkoa mmoja yaani Moro United wanakipiga na Polisi Morogoro
Simba na Ashant United tayari zimeshafuzu kwa sita bora huku Polisi Dodoma ikiwa inaongoza kituo cha Arusha na JKT Ruvu nao wanaongoza kituo cha Dodoma na Mtibwa Sugar wao wanafuaatia wakiwa wapili katika kituo hicho cha Dodoma

हस्र kwa कम्पुनी या सिमू

Kampuni ya simu Tanzania-TTCL nyanda za juu kusini magharibi imepata hasara ya shilingi Bilioni 2.2 kutokana na wizi wa nyaya za simu na vipuri mbalimbali kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hayo yamesemwa na meneja wa kanda hiyo Bwana SAIDI AMIR wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mjini MBEYA. Amesema maeneo yaliyokumbwa na kuibiwa nyaya hizo na kusababisha wateja wake kukosa mawasiliano ni pamoja na mikoa ya RUVUMA,MBEYA,RUKWA na IRINGA

Tuesday, 24 April 2007

Zambia na Libya zakubali kukipiga na Taifa Stars

Wauza mitumba washikwa shati

Baada ya ajari kuongezeka vidhibiti mwendo vyakumbukwa

Chama cha wamiliki wa mabasi nchini-TABOA kimewaagiza wamiliki wa mabasi yote kuhakikisha kuwa mabasi yao yana vidhibiti mwendo vinavyofanyakazi.
Kimesema wakati serikali inafanya jitihada za kutafuta njia mbadala ya kudhibiti mwendo kasi vidhibiti mwendo vilivyopo kwenye mabasi kwa sasa ndio viendelee kutumika.
Agizo hilo limetolewa Mjini DAR ES SALAAM na Mwenyekiti wa Taifa wa TABOA Bwana MOHAMMED ABDULLAH mara baada ya kukutana na Makamanda wa usalama barabarani wa mikoa yote nchini kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha usafirishaji wa abiria.
Katika taarifa yake Bwana ABDULLAH pia amewaagiza abiria wa mabasi hayo kumkemea dereva anayeendesha vibaya ikiwa ni pamoja na kwenda mwendo wa kasi.
Amesema, endapo dereva huyo atakaidi, watoe taarifa ya dereva huyo kwa mmiliki wa basi au kwa polisi wa usalama barabarani.
Mwenyekiti huyo wa chama cha wamiliki wa mabasi nchini amewashauri abiria wote nchini kuwa na utamaduni wa kudai tiketi inayoonyesha nauli anayotozwa, namba ya kiti, sehemu atokayo na aendayo.
Bwana ABDULLAH amesema, endapo kutakuwa na ushirikiano kati ya abiria, wamiliki wa mabasi na askari wa usalama barabarani, usafiri kwa njia ya barabara utaimarishwa na hivyo kupunguza ajali za barabarani.

Kumbe Watanzania wapo makini

Ni muda kidogo umepita toka Ugonjwa wa homa ya bonde la Ufa (RVF)uingie hapa Nchini ambapo watu waliambiwa kuwa wasile nyama ya Ng`ombe na Nyama ya Mbuzi ilikuepuka ugonjwa huo ni kweli watu hawali nyama kabisa
Ni muda kidogo umepita toka walipotoa tangazo hilo na hadi hii leo huwezi kuamini bado wananchi waliowengi hawali kabisa nyama hizo
Ukipita katika mabucha ya Nyama hasa hapa Dar Es Sallam utakuta nyama zikiwa zimewekwa huku wanunuzi ni wachache mno na hata baadhi ya mabucha yamefungwa kwa kukosa wateja wa kununua nyama hizo
Mfakazi mmoja wa bucha moja la Nyama hapa DSM ameuambia mtandao huu kuwa ni hivi sasa kazi ni ngumu mno kwamaana hakuna wateja kabisa wa kununua nyama
Biashara haiendi kabisa yaani wateja hakuna tunaleta nyama hapa Buchani lakini hakuna wa kununu ameeleza mfanyakazi huyo wa hilo bucha
Hongera Watanzania kwa kuwa makini na kuuepuka ugonjwa huo RVF, lakini tusiishie kwenye RVF tu pia tuwemakini hata kwenye ugonjwa hatari wa UKIMWI
Watu wanavyoogopa kula nyama hivi sasa wakihofia kukumbwa na RVF basi tuogope ngono uzembe ilitusipate Ukimwi kwamaana ni hatari zaidi kuliko RVF
Mtu asifanye mapenzi kabla ya ndoa asubiri hadi wakati wake ukifika pale atakapokuwa kwenye ndoa na waliokuwa kwenye ndoa basi waziheshimu ndoa zao wasitoke ovyo kwamaana ni hatari(UKIMWI NI HATARI kuliko RVF sasa tusiogope tu kula nyama hata Ngono tuogope hivyohivyo

Vita nyingine tena bara Ulaya

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa bara Ulaya kati ya Manchester United na AC Millan unachezwa leo usiku katika uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza
kocha wa Man Utd Sir Alex Ferguson anamatumani makubwa ya timu yake kufanya vyema katika mchezo huo ingawa timu yake inakabiliwa na majeruhi kibao ambao wataukosa mchezo wa leo dhidi ya AC Millan ya Italia
wachezaji wa Man Utd ambao wataukosa mchezo wa leo ni Rio Ferdinand Garry Neville, Nemanja Vidic, Mikael Silvestre, Craig Cathcart, Louis Saha, Ji-Sung Park na Kieran Richardson huku kukiwa na wasiwasi kwa mlinzi wa kushoto Patrice Evra kama anakuwa fit basi itamlazimu akae bechi
Sir Ferguson anasema ingawa baadhi ya wachezeji wake mahili wataukosa mchezo huo yeye bado anamatumaini makubwa na kikosi chake kuifunga AC Millan hii leo
Kwa upande wa AC Millan wao hawana matatizo ndani ya kikosi chao ambapo kocha mkuu wa timu hiyo Carlo Ancelotti ameondoka na kikosi kamili kwenda nacho nchini Uingereza kuivaa Manchester United akiwemo mshambuliaji Alberto Gilardino ambae alikosa mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali dhidi ya Buyern Munich ya Ujerumania alipokuwa akitumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano
kocha huko wa AC Millan Carlo Ancelotti amemjumuhisha katika kikosi chake kipa namba moja wa timu hiyo Nelson Dida inagwa anahatihati ya kuukosa mchezo huo kwa kuwa na maumivu ya bega lakini kocha huyo bado anamatumiani makubwa na kipa wake huyo kuwa anaweza kukaa lango(golini)
Manchester United na AC Milla zimewahi kukutana mara sita katika michuanoa hilo ambapo AC Millan imeshinda mara nne na Manchester United imeshinda mara mbili
Refa wa mchezo wa leo ni Kyros Vassaras kutoka nchini Ugiriki,kipute kitaanza saa 21 :45 kwa saa za Africa Mashariki
Michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itaendelea tena hapo kesho kwa mchezo baina ya Chelsea na Liverpool zote za Uingereza

Mnyama Simba azinduka bila Brazil

Michuano ya ligi ndogo ya shirikiso soka hapa Tanzania(TFF) iliyogawanywa katika makundi matatu ilishuhudia hapoa jana mnyama Simba akizunduka na kuitandika timu ya Tanzania Prisons kwa bao 3-0
Magoli yote ya timu ya Simba yalifungwa na kiungo wake mahili ambae ameonyesha kiwango kikubwa cha soka msimu huu Haruna Moshi(Boban) ambae hapo jana alicheza nafasi ya ushambuliaji akiziba nafasi ya mshambuliaji Joseph Kaniki anaetumikia adhabu ya kuwa na kadi nyekundu
Kocha msaidizi wa timu hiyo ambae hivi sasa amebakia peke yake baada ya kocha mkuu wa timu hiyo Mbrzil Nielsen Elias kuitema timu hiyo na kuondoka bila taarifa yeyote ile alisema vijana wake walicheza vizuri hapo jana baada kufuata maelekezo yake aliyoyatoa kabla ya mchezo
katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo matokeo yalikuwa ni sare ya kutofungana hivyo Simba wamejilekebisha na kufanikiwa kupata ushindio huo mkubwa wa magoli 3-0
katika kituo cha Dodoma timu ya Kagera Sugar nayo imezinduka baada ya kuifunga timu ya Pan Africa kutoka Dar Es Salaam(wazee wa mjini) bao 1-0 ,bao hilo peke la Kagera Sugar lilifungwa na Paul Ngwai katika dakika ya tatu ya mchezo
Ligi hiyo ndogo inaendele tena leo katika kituo cha Morogoro kwa mchezo mmoja baina ya Polisi Dodoma ambayo itaumaana na timu ya Ashant United (wauza mitumba wa Ilala) ambayo hapo jumamosi mchezo wao na timu ya Simba ulivunjika baada ya kuzuka vurugu

Monday, 23 April 2007

Top 5 za Africa Mashariki kutoka PRT Radio

1 .Missing Ma baby - Amani
2.Si lazima tu do - Nonini
3.Cenderela - Ally Kiba
4.Sinanoma nae - Aman, Jua kali
5.Nakiboona - Juliana
Habari hizi ni kwa mujibu wa Radio Presenter wa PRT -Djaro Arungu
hizi chat ni kwa kila siku za Ijuma pia usikose kusikiliza PRT kila siku .pia usikose kipindi cha Ladha za Africa Mashariki kila siku za Jumatau,Jumatano na Ijuma ,muda ni saa 12:30 jioni hadi saa 2:oo usiku kutoka PRT

Carvalho na Ballack kuikosa Liverpool

Wachezaji wawili mahili wa timu ya Chelsea Michael Ballack na Racrdo Carvalho wapo katika hatihati ya kucheza mchezo wa kesho kutwa wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya timu ya Liverpool
Hadi hivi sasa tayari viongozi wa timu hiyo wanonyesha kukubali kumkosa mlinzi huyo wa kati raia wa Ureno lakini wanajairibu kuangalia nini kifanyike kwa kiungo mahiri kutoka nchini Ujerumani
Michael Ballack aliumia siku ya jumapili kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle ambapo timu hizo zilitoka suluhu ya kutofungana ambapo kiungo huyo alijitinesha enka yake
Pigo hilo la kumkosa Ballack itakuwa ni kumtonesha maumivu kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ambae tayari ameshamkosa kiungo raia wa Ghana ambae ataukosa mchezso huo dhidi ya Liverpool kutokana na kutumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano
katika safu ya ulinzi wa kati Jose Mourinho amebakiwa na nahodha wake tu John Terry hivy kuwa na kazi nyingine ya kutafuta msaidizi wa kumsaidia nahodha huyo ambapo sasa analazimika kumtumia Khalid Boulhrouz au Paulo Ferreira ili kusaidiana na John Terry ilikuweza kuzuia mashambulizi ya Liverpool hapo Jumatano usiku
Ukiondoa tatizo la wachezaji wake kuwamajaruhi sasa kunakingine Mourinho kinawezakumba kwenye mchezo wa marudiano nacho ni kunawachezaji wake wengi wanakadi moja ya njano baadhi yao ni Didier Drogba ,John Terry , John Mikel Obi nk
kama watapata kadi nyingine hapo kesho kutwa basi watakosa mchezo wamarudiano

Gattuso aitaman Man Utd

Kiungo machachali wa timu ya AC Millan ya Italia – Genaro Gattuso amesema kwamba anavutiwa sana na kocha wa timu ya Manchester United - Sir Alex Ferguson pamoja na timu hiyo
Genaro Gattuso anasema kesho atajitahidi kucheza soka la uhakika iliaweze kumshawishi kocha huyo aendeleze mikakati yake ya kumnyakuwa mwisho mwa msimu huu
Kunamawasiliano kati yetu yanaendelea lakini kwasasa ninaangalia nini ninafanya kwaajili ya timu yangu ya AC Millan hasa kwenye mchezo wa kesho wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ULAYA amesema Genaro Gattuso
Genaro Gattuso amekili kwamba ni kweli anandoto ya siku mmoja acheze soka nchini Uingereza na timu anayotaka kuichezea ni Manchester United si nyingine pia a anapendezwa sana na hari ya hewa ya nchi hiyo na kufutiwa na soka linalichezwa kuliko la nchini kwao ITALIA

Ferguson awapamba Ronaldo na Kaka

Kocha wa timu ya Manchester Unieted Sir Alex Ferguson amesema kwamba hapo kesho wachezaji bora zaidi hapa ulimwenguni kwa sasa Cristiano Ronaldo na Ricardo Kaka watakutana kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya
Mchezo huo wa kwanza wa nufu fainali ya michuano hiyo utapigwa nchini UINGEREZA kwenye uwanja wa Old Trafford nyumbani kwa Manchester United
Ninaweza kusema kwamba kwa sasa hakuna wachezaji bora zaidi hapa Duniani kama Cristiano Ronaldo na Ricardo Kaka ameendelea kusema Sir Ferguson, kwamaana Ronaldo amekuwa bora na msaada mkubwa katika msimu huu kwa Manchester United na Kaka hivyo hivyo kwa timu yake ya AC Millan
Kunawachezaji wengine bora kwenye timu zote mbili kama Paolo Maldini lakini hao wawili ni zaidi na ninahakina mchezo huo utakuwa mgumu mno na ninawaambia AC Millan kuwa Manchester United ya msimu huu ni nzuri kupita ya mwaka 2005 waliyoitoa kwenye hatua ya pili na wategeme upinzani wa kweli hakuna wepesi amesema Sir Alex Ferguson

NGOMA BADO NGUMU.




NI BAHATI KWA MAN UTD KWANI MPAKA SASA BADO WANAENDELEA KUONGOZA LIGI, LAITI CHELSEA WANGEPATA USHIDNI KATIKA MECHI YA JANA DHIDI YA NEWCASTLE HII LEO WANGEKUWA WANAZUNGUMZA MENGINE.

LAKINI MECHI BADO ZIPO HUENDA WAKATIMIZA MALENGO YAO YA KUTETE TAJI LA UINGEREZA.