Tuesday, 1 May 2007

Nani mtemi hii leo baina ya Liverpool na Chelsea

Ni mara nyingine tena timu mbili za nchini Uingereza za Liverpool na Chelsea zinamumaana kwenye mchezo wa marudianao wa ligi ya mabingwa barani Ulaya
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa Chelsea mabilione hao walifanikiwa kuifunga Liverpool bao 1- 0,bao lilofungwa na kiungo mchambuliaji Joe Cole
Mchezo wa leo unapigwa kwenye uwanjwa wa Anfield nyumbani kwa Liverpool huku wenyeji hao wakiwa na matumaini makubwa kurudi yake walioyafanya mwaka 2005 ambapo walifanikiwa kuitoa Chelsea kwenye michuno hiyo baada ya kuinyuka baoa 1-0,bao lilotiwa kimiani na Luis Gacia
Hii leo Chelsea itaingia dimbani bila la kiungo wake rai wa Ujerumani Michael Ballack aliemajeruhi na mlinzi wa kati Ricardo Carvslho ambae nae ni majeruhi hinyo kumfanya kocha wa Chelsea Jose Mourinho kuumia kichwa
Katika hatua hiyo Mourinho atalazimika kumtumia kiungo wa Ghana Michael Essien kama m linzi wa kati akishirikia na John Terry ilikuweza kulinda ngome ya timu hiyo pamoja na kulinda ushindi wao wa goli moja walioupata nyumbani kwao
Kunauwezekana pia mshambuliaji hatari wa timu ya Chelsea raia wa Ukrain Andriy Shevchenko akaukosa mchezo wa leo kutokana na maumivu ya misuli hivyo kuzi kumuumiza Jose Mourinho
Kwa upande wa Liverpool wao hawana amatatizo kabisa kwamaana kikosi chao chote ni kizima na hakina matatizo yeyote yake
Na kocha wa Liverpool Rafael Benitez amejigamba kuwa lazima waitoe timu hiyo kwamaana wamejianda kikamilifu na wanahamu tena ya kucheza fainali ya michuno hiyo kama walivyofanya mwaka 2005

1 comment:

Anonymous said...

OYA BWANA MDOGO ACHA HIZO YAAANI ILIIONA HIYO TU NINI CHELSEA UKWELI NI KWAMBA NDUGU UINGEREZA PANA VILABU VIWILI TU, ARSENAL NA MAN UTD WENGINE TWAWEZA KUWAITA WAVAMIZI.

USIKASIRIKE HAYO NI MAWAZO TU NDUGU YANGU, UNAJITAHIDI KAZA UZI WA KUIBORESHA BLOG YAKO, HONGERA SANA NDUGU YANGU DAIMA UKWELI UTABAKI PALE PALE HAKUNA KLABU KAMA MAN UTD NA ARSENAL UINGEREZA HAO CHELSEA NI INTRUDERS TU, NA WAUSAHAU UBINGWA WA UINGEREZA SASA, HAWANA JIPYA YAANI HATA ARSENAL WALIWAKOSA KOSA HAMA MZEE HAPO UNAJIDANGANYA!!!!!!!!!!!!!!