Ama kwa hakina mpenzi wa soka huwezi kuamini timu ya Simba imeshindwa kulipa kiasi cha shilingi 140000 za kitanzania kwa ajiri ya kulipia Hostel waliyokuwa wakikaa kwa kipindi cha wiki mbili za mashindano ya ligi ndogo ya TFF
Habari kutoka Morogoro zinasema kwamba wachezaji wa timu hiyo waliluhusiwa kuondoka kwenye Hostel za chuo kikuu cha Waislamu mkoani humo lakini gari la kingozi mmoja wa timu hiyo ya Simba aina ya Toyota Prado namba T276ABX limezuhiliwa hadi pale viongozi wa timu hiyo ya Simba watakapolipa deni hilo
Mmoja wa viongozi wa Hostel hiyo ameuammbia mtandao huu kuwa kwa kipindi cha wiki zote mbili walizokaa pale ni wiki moja tu viongozi wa timu hiyo walilipa kodi lakini wiki nyingine moja hawakulipa kodi na walitaka kuwazuia na wachezaji wa timu hiyo wasiondoke lakini wamemua kuwaachia na kulizuia gari hilo hadi pale watakapopata pessa zao
Katika Hostel hiyo Simba walikuwa wakipata huduma mbalimbali kama vile chakula na uwanja wa kufanyia mazoezi na kila kitu walitakiwa kukilipia lakini wao hawakulipa na viongozi wa Hostel hiyo waliwaamini sana viongozi wa timu hiyo lakini hivi sasa uaminifu wao umekwisha
Hapo jana timu ya Simba walicheza mchezo wao wa mwisho wa michuano hiyo ya ligi ndogo dhidi ya Ashant United na kupokea kipigo cha bao 2-0 hivvo kumaliza michuno hiyo wakiwa wa pili nyuma ya wauza mitumba hao kutoka mitaa ya ILALA hapa Dar es salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
U cant imagine that this is the so called 'timu tajiri ktk bongo'.. yaani 140k? noma!
Post a Comment